• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo

Wajumbe wa ALAT Wapata somo la Mifumo

Imewekwa tar.: September 27th, 2018


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania Bara (ALAT), wamepata somo juu ya mifumo inayo simamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) na jinsi mifumo hiyo ilivyo saidia katika masuala mtambuka ya kimaendeleo katika jamii.

Somo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa TEHAMA OR TAMISEMI, Ndugu Erick Kitali wakati wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya hiyo unaoendelea mkoani Dodoma na kuwakutanisha wajumbe kutoka Halmashauri 185 za Tanzania Bara.

Akitoa mada hiyo Mkurugenzi huyo wa TEHAMA, alisema toka kuanza kwa mifumo mambo mengi yameimarika ikiwepo suala la mapato ya halmshauri ambapo kupitia mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri (Local Government Revenue Collection Information System- LGRCIS), imewezesha halmashauri hizo kujiongezea mapato ya ndani ikilinganishwa na hapo awali.

“Waheshimiwa wajumbe, kupitia mifumo yetu hali ya makusanyo imeongezeka sana ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambacho tulikuwa tunakusanya kwa risiti za kawaida” alisema Kitali, na kutolea  mfano katika maeneo yetu ya kutolea huduma za afya hususan ni katika Hospitali za Wilaya ambapo makusanyo yalikuwa kati ya Mil. 3 hadi 6 kwa mwezi, lakini pindi matumizi ya mifumo yalipoanza, makusanyo yamepanda na kufikia Mil. 24 hadi 40 kwa mwezi.

Kwa upande wao wajumbe hao wakichangia na kutoa ushauri walipongeza kazi nzuri inayofanywa na wizara ya OR-TAMISEMI, huku wakitaka maboresho ya mtandao katika mifumo hiyo iweze kuongeza ufanisi hasa katika maeneo ya pembezoni mwa nchi, ambapo mkonga wa taifa bado haujafika.

Akichangia mada Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba, alisema katika kuimarisha suala zima la Makusanyo Serikali iende mbele na kuwa na mawazo mbadala juu ya (Point of Sell- POS).

“Mhe. Mwenyekiti nadhani umefika wakati wa kuwa na mashine hizi za POS ambazo zitakuwa zinajazwa Flot ili kusaidia kuepusha hatari mbali mbali ikiwepo kukwepa wajanja wanao chezea mashine lakini vile vile hali ya hatari yakupoteza mashine.” alisema Kibamba.

Katika wasilisho hilo lililopata wachangiaji wengi, Mkurugenzi Erick hakucha kuwashukuru wadau mbali mbali ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa mawazo mbadala yakuboresha mifumo.

“Kufanya kazi  OR-TAMISEMI, haina maana ndio utakuwa unaelewa kila kitu, huu ni mpangilio tu wa majukumu, sisi kama wataalam ndani ya Wizara tunapokea mawazo yenye kujenga ili shabaha yetu yakuwahudumia wananchi iweze kufikiwa hivyo tunapokea mawazo yenye tija na kuyafanyia kazi kwa manufaa ya taifa” alisema Kitali.

Wasilisho hilo ambalo liliwasilishwa katika mkutano huo wa 34, lilihusiaha mifumo ya  Tovuti za Mikoa na Halmashauri (Government Website Framework GWF), ambao upo kwenye Halmashauri 185 na mikoa 26 nchini, mfumo wa Malipo unatumiwa na halmashauri (Epicor) na  mfumo wa Mipango na bajeti (Planning Budgeting and Reporting PlanRep).

Mifumo mingine iliyo wasilishwa katika kikao hicho ni Mfumo wa taarifa za Shule (School Information System SIS), mfumo wa Vibali vya kusafiria nje ya nchi (eVibali), Mfumo wa kukusanya, kuchambua na kutoa taarifa ya takwimu ya Elimu Msingi (Basic Education Management Information System BEMIS), Mfumo wa Uhasibu na Utoaji taarifa kwa ngazi ya kituo (Financial Facilities Account and Reporting System FFARS) pamoja na mfumo wa kukusanya, kuhifadhi na kutoa taarifa za kitabibu  (Government of Tanzania Health Management Information System GoTHoMIS).

Mkutano mkuu wa wa 34 wa Jumuiya ya Mamlaka za Mitaa ALAT,unafanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na umewashirikisha Wenyeviti,Mameya, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, watendaji kutoka OR-TAMISEMI pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo waliopata mialiko ya mkutano huo.

Anaandika Atley Kuni- OR TAMISEMI.



Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.