• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

TAMISEMI YAWASILISHA BAJETI ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI SABA

Imewekwa tar.: April 19th, 2021

Na Fred Kibano – Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo Jijini Dodoma leo ambapo zaidi ya shilingi trilioni saba zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya wizara hiyo, Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zilizo chini yake katika mwaka wa fedha 2021/2022.

“Mheshimiwa Spika, sasa naomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya Shilingi Trilioni Saba Bilioni Mia Sita Themanini na Tatu Milioni Mia Tatu Ishirini na Tisa Mia Sita Arobaini na Nne Elfu na Mia Nane, Shilingi 7,683,329,644,800.00, kwa ajili ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Fungu 56, Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu Na. 2 na Mafungu 26 ya Mikoa yanayojumuisha Halmashauri 184”

Waziri Ummy Mwalimu amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Taasisi zilizo chini yake, Mikoa 26 na Halmashauri 184 zinatarajia kukusanya Maduhuli na Mapato ya ndani jumla ya shilingi 916,445,409,198 na kwamba makusanyo hayo yatatokana na mauzo ya vifaa chakavu, ada za wanafunzi, tozo mbalimbali na ushuru unaotozwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kulingana na sheria ya fedha za Serikali za Mitaa.

Vilevile, amesema katika mwaka wa fedha 2021/22, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imepanga kutekeleza malengo mahsusi kama vile kuimarisha na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma vilivyokamilika vinaanza kutoa huduma za Afya na Elimu ikiwa ni pamoja na ununuzi wa dawa, vitendanishi, vifaa na vifaa tiba na utengenezaji wa madawati kwa Shule za Msingi na Sekondari sambamba na kujenga vituo vya afya vipya 121 kwa gharama ya Shilingi bilioni 60.50 kwenye Halmashauri nchini pamoja na malengo mengine.

Ameliambia Bunge kuwa awamu ya Kwanza ya ujenzi wa shule 10 kati ya shule 26 za Sekondari za wasichana za bweni kidato cha tano hadi cha sita kwa masomo ya Sayansi, shule moja kwa kila Mkoa zimeanza kujengwa na zitakapokamilika zitakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita na wanafunzi kati ya 1,000 hadi 1,31 1,200 kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 40 zimetengwa.

Aidha, Serikali itaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri ambapo shilingi bilioni 67.66 ambazo ni fedha za ndani zimetengwa kwa mwaka ujao wa fedha.

Kuhusu ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa gharama ya Shilingi bilioni 627.044 zimetengwa ambapo Shilingi bilioni 272.50 zinatokana na Mfuko wa Barabara, Shilingi bilioni 127.50 zinatokana na Mfuko Mkuu wa Serikali na Shilingi bilioni 12.75 zinatokana na Mapato ya Ndani ya TARURA ambapo jumla ya kilomita 136.82 barabara za lami, kilomita 500 za barabara za changarawe na Kalvati/ madaraja 90 yatatengenezwa.

Waziri Ummy amesema taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2019/20 imebainisha kwamba Halmashauri 124 sawa na asilimia 67 zimepata Hati Zinazoridhisha (Hati Safi), Halmashauri 53 sawa na asilimia 29 zimepata Hati Zenye Shaka na Halmashauri 8 sawa na asilimia 4 zimepata Hati Zisizoridhisha (Hati Chafu).

Amesema matokeo ya ukaguzi yanaonesha kutofanya vizuri kwa Halmashauri nyingi ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2018/19 ambapo Halmashauri zilizopata Hati Zinazoridhisha zilikuwa 176 sawa na asilimia 95 na Hati Zenye Shaka Halmashauri 9 sawa na asilimia 5. Hapakuwepo na Halmashauri zilizopata Hati Chafu na hivyo kuahidi kufuatilia Halmashauri zilizofanya vibaya.

“Ofisi ya Rais TAMISEMI itazifuatilia na kuzisimamia Halmashauri zote ili kuhakikisha kwamba masuala yote yaliyobainishwa na CAG yanafanyiwa kazi kikamilifu ikiwemo kuchukua hatua kwa watumishi wote wa Halmashauri ambao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo au kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy Mwalimu amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Wadau wa Maendeleo katika utekelezaji wa Programu, Miradi na shughuli mbalimbali za Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambao ni pamoja na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA), Jumuiya ya Ulaya (EU), Global Partnership for Education, Shirika la Maendeleo la Uingereza (Foreign, Commonwealth and Development Office FCDO), Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID), Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Nchi zinazochangia kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya ambazo ni Denmark, Ireland, Jamhuri ya Korea (KOICA) na Switzerland.

Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI inatarajiwa kujadiliwa kwa siku tatu kabla ya Bunge kuridhia na kupitisha mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022

Hotuba ya Ofisi ya Rais TAMISEMI inapatikana kupitia tovuti ya www.tamisemi.go.tz


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.