• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Silinde Aagiza Maafisa Elimu Kata Kusimamia Miradi ya Maendeleo kwa Weledi

Imewekwa tar.: April 9th, 2021

Na. Fred Kibano na Asila Mohammed Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) David Silinde amewaagiza Maafisa Elimu Kata nchini kusimamia rasilimali fedha za miradi ili kuongeza tija kwenye sekta hiyo muhimu hapa nchini.

Akifungua kikao kazi kilichowakutanisha Maafisa Elimu Kata Tanzania Bara ambao agenda kuu ni kuunda umoja wao wa WARATIBU ELIMU KATA TANZANIA BARA (UMEKTA) Jijini Dodoma hii leo,Silinde amesema miradi mingi kwenye sekta ya elimu haikamiliki kwa wakati na hivyo jamii inayoizunguka miradi hiyo kuchelewa kupata manufaa ya miradi hivyo hakuna budi Waratibu Elimu Kata wahusishwe moja kwa moja na kwamba baadhi yao wanazembea na kuisababishia Serikali hasara.

“Kuhusu usimamizi wa fedha na miradi ya elimu, kila Afisa Elimu Kata asimamie miradi na fedha zote za Serikali ndani ya kata yake kwa shule zote za msingi na sekondari” alisema Silinde

Aidha, Silinde amesema hali ya uandikishwaji imeongezeka na hili ni kutokana na Serikali kutoa Elimu Bila Malipo hivyo kuwataka Maafisa hao kuwajibika katika kusimamia elimu katika maeneo yao.

Kuhusu taaluma amewataka kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala la elimu ya Ufundishaji na Ujifunzaji wa wanafunzi nchini kwenye shule za msingi na sekondari akiwaasa baadhi ya Maafisa Elimu Kata kutowajibiki katika usimamizi wa shule za sekondari katika maeneo yao na kusababisha kutokuwa na taarifa muhimu za kielimu lakini pia watakaowakwamisha kusimamia elimu ya sekondari watolewe taarifa ili hatua stahiki zichukuliwe.

Pia amewataka viongozi hao kulisimamia suala la ufundishaji na ujifunzaji (KKK) na Elimu ya Awali linakuwa kipaumbele kwao kwa kuhakikisha wanalisimamia ili kujua changamoto zinazowakabili wanafunzi.

Katika hatua nyingine, Silinde amewaagiza maafisa hao kutumia mifumo kwa kuhakiki taarifa mbalimbali zinazoingizwa kwenye mifumo kama vile SIS, PReM na PReMs ili kuepuka  kuingiza taarifa ambazo zisizo sahihi


Kwa upande wake Gerald Mweli ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) ametoa rai kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuwajengea uwezo na kuwaamini maafisa hao katika eneo la rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na rasilimali fedha na pia amewataka maafisa hao kutunza pikipiki walizopatiwa na Serikali kwa lengo la kukagua taaluma kwenye maeneo yao na kuipaisha sekta ya elimu nchini.

Mweli amesema pia shule za msingi zimeongezeka kutoka 16,899 waka 2015  hadi 17,804 mwaka 2020 na shule za sekondari kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi 5,330 mwaka 2020 wakati vyumba vya madasa kwenye shule za msingi kutoka 115,665 mwaka 2015 hadi 136,292 mwaka 2020.

Naye Robert Tesha ambaye ni Mwenyekiti wa Waratibu Elimu Kata Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya washiriki wote ameahidi kutimiza wajibu wao ili kuinua kiwango cha taaluma nchini pia watajadili mambo muhimu yanayohusu katiba kwa muda wa siku mbili yatakayosaidia umoja huo uanze kufanya kazi mara moja.

“tuna ahidi kutimiza wajibu wetu ili kuinua kiwango cha elimu nchini kwani changamoto nyingi zilizokuwa zinatukabili zimefanyiwa kazi kama kulipwa posho na kupatiwa pikipiki hii imeongeza ufanisi wa kutimiza wajibu wetu”  

Akitoa neno la shukrani, Paul Kamele Mwenyekiti wa Waratibu Elimu Kata Mkoa wa Morogoro amesema jukwaa la maafisa hao lilikuwa liwe limeanza kwa muda mrefu ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

‘’Katika kipindi hiki ambapo tunafanya sensa ya mwaka ya elimu kila mmoja ahakikishe taarifa zinazoingizwa kwenye dodoso ni sahihi’’ amesisitiza Silinde.

Kikao hicho cha siku mbili kilihudhuriwa na Maafisa Elimu Kata Tanzania Bara, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Chama cha Walimu Tanzania, Tume ya Utumishi ya Walimu na Maafisa Elimu Wilaya hapa nchini.


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.