• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali yazionya shule binafsi ziache kukataza wazazi kutembelea mabweni ya wanafunzi

Imewekwa tar.: September 19th, 2018

Na Mathew Kwembe, Dodoma

Serikali imezionya baadhi ya shule binafsi nchini zenye tabia ya kuwakataza wazazi wenye watoto wanaokaa kwenye mabweni kuwatembelea watoto wao mabwenini ili kuona mazingira halisi wanayoishi watoto wao.

Aidha Serikali pia imepiga marufuku mtindo wa baadhi ya shule binafsi ya kutofuata utaratibu uliowekwa na serikali wa watoto kufanya mtihani wa kidato cha pili baada ya kusoma sekondari kwa miaka miwili badala ya wao kulazimisha wasome kwa mwaka mmoja na miezi minne tu.

Akifunga kikao kazi cha watendaji wa elimu ngazi za Mikoa na Halmashauri jana jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt Leonard Akwilapo alisema kuwa umeibuka mtindo wa baadhi ya shule binafsi nchini kuwakataza wazazi wanaowatembelea watoto wao wanaokaa kwenye mabweni kutoingia katika mabweni hayo ili wajionee mazingira halisi wanayoishi watoto wao.

Alisema shule hizo binafsi hazina sababu za msingi za kufanya hivyo, kwani wazazi wana jukumu la kufahamu mazingira halisi wanayopaswa kuishi watoto wao shuleni, na hivyo alizionya shule za binafsi zenye mtindo huo kuacha mara moja.

Dkt Akwilapo aliongeza kuwa zipo baadhi ya shule binafsi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wanafunzi kutokana na kuwa na mazingira mabaya shuleni hasa kwenye mabweni ya wanafunzi na hivyo Wizara ya Elimu kupitia Kitengo cha Udhibiti Ubora wamekuwa wakizifungia shule hizo hadi marekebisho muhimu yafanyike.

“Katika shule za ‘private’ wazazi wanakatazwa wasitembelee mabweni kuona mazingira wanayoishi watoto wao, ni haki ya mzazi kujua mtoto anakaa wapi,” alisema.

Hivyo, Katibu Mkuu huyo aliwataka Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa shule za binafsi zinatekeleza agizo hilo ili watoto waweze kusoma wakiwa katika mazingira mazuri ya mabweni.

Akitolea mfano wa kufungwa kwa mabweni katika shule ya sekondari ya Kigurunyembe ya mjini Morogoro, Dkt Akwilapo alisema kuwa Wizara ilazimika kuyafunga mabweni ya shule hiyo kwani yalikuwa katika mazingira mabaya sana.

Jambo lingine alilolitolea maelekezo ni suala la baadhi ya shule binafsi ya kutofuata utaratibu uliowekwa na serikali wa watoto kufanya mtihani wa kidato cha pili baada ya kusoma sekondari kwa miaka miwili badala yake shule hizo zimekuwa zikilazimisha watoto hao wasome kwa miezi minne tu mara baada ya kufanya mtihani wao wa darasa la saba kwa kisingizio kuwa watoto hao wana vipaji maalumu.


Alisema baadhi ya shule binafsi zimekuwa na mtindo wa kuwafundisha watoto  wanaomaliza darasa la saba kwa miezi minne badala ya mwaka mmoja kwa masomo yote ya kidato cha kwanza.

“Wakishasoma kwa miezi minne, kuanzia septemba hadi disemba ikifika mwezi januari,  wamiliki wa shule hizo hulazimisha baraza la mitihani wawaandikishe wanafunzi hao ili wafanye mtihani wa kidato cha pili, nawaagiza mwende mkalisimamie  na mkemee tabia hii,” alisema

Mbali na maagizo hayo Dkt Akwilapo aliwataka maafisa elimu hao kwenda kushirikiana na halmashauri zao kuhakikisha kuwa wanaongeza madarasa na pia maabara kwa shule za kidato cha tano na sita.

Alisema wizara yake ililazimika kuzikatalia baadhi ya halmashauri zilizokuwa zikitaka ziwe na shule za kidato cha tano na sita kwa kuwa zilikosa kuwa na ubora hasa kwa kutokuwa na madarasa ya kutosha, matundu ya vyoo ya kutosha, mabweni yaliyo katika mazingira bora na sehemu za kupikia zisizoridhisha.

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Tixon Nzunda alisema kuwa kikao hicho kilikuwa ni muhimu kwa ajili ya kupeana taarifa na maelekezo kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya ambao wengi wao ni wapya.

Alisema kuwa katika kikao kazi hicho, suala la kuzingatia misingi ya maadili ya kazi na nidhamu yalipewa kipaumbele karibu katika mada zote  zilizotolewa.



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.