• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali Yatoa Miezi 3 Ukamilishaji Vituo vya Afya 98

Imewekwa tar.: July 10th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jafo (Mb) ametoa siku mia moja na ishirini na tatu (123) kuanzia leo (tarehe 10 Julai, 2018) kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote zilizo pokea fedha za awamu ya tatu ya ukarabati wa vituo vya afya ziwe zimekalisha ujenzi huo.

Mhe. Waziri Jafo ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kukagua Vituo vya afya vinavyo endelea kujengwa nchi nzima.

Katika ziara hiyo, mkoani Singida  Mhe. Jafo amekagua kituo cha Afya Kintinku kilichopata fedha katika awamu ya kwanza milioni. 500  na kuridhishwa na hali ya ujenzi akiwa ziarani alipata pia wasaa wa kukagua eneo la ujenzi wa kituo cha Afya cha Nkonko kilichopokea Mil. 400 ambacho kitakarabatiwa na kuongezewa majengo manne.  

Mhe. Jafo alisema, fedha hizo zitatumika kukarabati jengo la mama na Mtoto, Jengo la upasuaji, Maabara sambamba na nyumba ya Mtumishi katika Kijiji hicho.

“Mil. 400 mlizopokea hapa kituo cha afya Nkonko, nataka ifikiapo Oktoba 30, 2018 ziwe zimefanya kazi nzuri kuzidi ile ya Kintinku” alisisitiza Waziri Jafo na kuongeza kwamba, zoezi hilo sio kwa Nkonko peke yake bali Halmashauri zote zilizo pokea fedha za awamu ya  tatu inayo husisha vituo vya afya 98.

Mhe. Jafo, Waziri mwenye dhamana na OR TAMISEMI, akitoa salaam za Mhe. Rais, alisema nia ya Serikali ya awamu ya tano ni pamoja na kumkomboa Mwananchi hususani kwa kumsogezea huduma bora za kijamii jirani.

“Ndugu zangu kabla yakuendelea na hutuba yangu, naomba nilete salaam za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhe. Rais anasema anawapenda sana na anawashukuru kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuongoza Nchi yetu, yeye amesema atawalipa fadhila kwa kuwatumikia kwa nguvu zake zote na kuhakikisha huduma za jamii zinakuwa bora ikiwepo suala la afya.” Alisema Waziri Jafo na kuongeza kwamba, wananchi waendelee kumuombea ili kazi waliyompatia kwa miaka yake ya uongozi yeye na wasaidizi wake waweze kuikamilisha” alinukuliwa Waziri Jafo.

Mbali na kutoa salaam za Mhe, Rais Mhe. Waziri Jafo hakusita kuelezea jinsi Mbunge wa  Jimbo hilo la Manyoni Mashariki Mhe. Daniel Mtuka, anavyo pigania maendeleo ya jimbo lake,  Mhe. Waziri Jafo amewaambia wananchi wa Jimbo la Manyoni Mashariki kwamba siku zote Mbunge wao amekuwa akikumbushia suala la ukarabati wa kituo cha Nkonko na Kintunku vilivyopo katika Jimbo lake.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu ambaye pia anakaimu nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Manyoni, aliye Mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida katika ziara hiyo, alimuhakikishia Mhe. Waziri wa Nchi juu ya usimamizi madhubuti wa fedha hizo na kwamba hata kuwa na mzaha na yeyote atakayejaribu kwenda  kinyume na makusudio ya fedha hizo.

“Mhe. Waziri mimi nikuhakikishie kwamba, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kuwa, kila shilingi itakayotumika katika ukarabati wa majengo ambayo imeletwa kwa ajili ya kituo hiki itafanya kama ilivyo kusudiwa na kwa mtu atakayethubutu kwenda tofauti hatutakuwa na huruma naye lazima mkondo wa sheria uchukue nafasi yake” alisema Mtaturu.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Daniel Mtuka, alisema wananchi hao wapo tayari kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ubora na kuzingatia thamani halisi ya fedha iliyotolewa.

“Nadhani Mhe. Waziri umekiona tulicho kifanya katika kituo cha afya Kintinku, sasa kwa moto ule ule chini ya Mkuu wetu wa Wilaya kijana wetu Mhe. Mtaturu anaye Kaimu kwa sasa nafasi ya Ukuu wa Wilaya, ambaye kwa kweli kama alivyo sema mwenyewe, mtu atakayejaribu kukwamisha shughuli za mradi huu atakwenda jela na hata muonea haya mtu wa aina hiyo”.

Mtuka alisema Mtaturu alisimama kidete Kintunku na wanaimani atasimamia vema na kutoa maelekezo sahihi katika kituo hicho cha Nkonko

Awali akiwa katika kituo cha Afya Kintinku, Waziri Jafo hakuacha kuwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kusema miongoni mwa Wilaya zilizofanya vizuri katika ukarabati wa vituo vya afya nchini ni pamoja na Kintinku.

“Leo Mhe. Rais anashuhudia katika vyombo vya habari, miongoni mwa watu mliofanya vizuri, watu wa Kintinku mmefanya vizuri sana sina budi kuwapongeza uongozi na wananchi kwa jumla jinsi mlivyo jitoa.” alisema Mhe. Jafo.

Wakizungumza kando ya mkutano huo wanachi katika maeneo ya Vijiji vya Kintunku na Nkonko wamepongeza jitihada zinazo chukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ya kuwaboreshea huduma za afya.

Serikali katika awamu ya tatu ya ukarabati wa vituo vya afya, imetoa jumla ya fedha za kitanzania Shilingi Bilioni 38.9 ambazo zimeelekezwa kwenye ujenzi wa vituo vya  afya vipatavyo 98 kote nchini.

Anaandika Atley Kuni- OR TAMISEMI

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.