• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo

Serikali yaagiza Kituo cha Afya Majengo kuhudumia wananchi

Imewekwa tar.: June 9th, 2018

Serikali imeagiza kuanza kutolewa kwa huduma za afya katika kituo cha afya majengo wilayani Nanyamba mkoani Mtwara ndani ya miezi mitatu kwa kuwa ujenzi wa majengo yake yote yapo katika hatua za mwisho.

Akitoa maagizo ya Serikali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula amesema hakuna haja ya kuchelewesha kutoa huduma za afya katika kituo cha afya majengo kwa kuwa wananchi wanahangaika kuitafuta huduma hiyo mbali wakati miundombinu ya kituo hicho ipo katika hatua za mwisho.

“kwa sababu watu wanahitaji huduma, wanafanya mawasiliano sehemu nyingine ili kupata huduma ambayo hapa haipo, lakini ndani ya miezi mitatu lazima huduma zianze kutolewa, Mganga Mkuu wa Wilaya Nanyamba andaa andiko ili mchakato wa kuanzisha kituo uanze mara moja”

Dkt. Chaula ametoa agizo hilo mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Nanyamba, Mganga Mkuu wa Mkoa Mtwara, wataalam wengine kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akiongea na wananchi katika mkutano ulioandaliwa baada ya kukagua miundombinu ya kituo cha afya majengo.

Aidha, Chaula amesema wakati Serikali inawapangia vituo watumishi wapya 6,180 imewaweka katika mpango wa kuwapangia vituo watumishi wapya katika vituo vipya vinavyokamilika kwa wakati, lakini pia ametoa angalizo kwa wananchi, watumishi na viongozi wote wilayani Nanyamba kuweka mazingira rafiki ili watumishi wapya wasipatwe na hali ya kuyakataa mazingira ya kazi bali watoe motisha kutatua changamoto hiyo.

Hassan Mnengu ni mwananchi wa kijiji cha majengo anasema huenda usumbufu waliokuwa wakiupata utakwisha kwa kufuata huduma za afya mbali na kijiji chao kwa hivi sasa.

“haya majengo yatatutatulia changamoto zilizopo, moja ya usumbufu ni wa kufuata huduma za afya kutoka Nanyamba kwenda wilaya ya Tandahimba au kituo cha afya kilichopo Nanguruwe”

Katika hatua nyingine, Dkt. Zainab Chaula amewaasa wananchi kupanda miti ya matunda zaidi badala ya miti ya kivuli ikiwa ni pamoja na maeneo ya vituo vya afya kwani ni sehemu ya lishe ya jamii.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, wilaya ya Nanyamba ina zaidi ya wakazi 114,000 na hivyo vituo vitatu vya afya wanavyovijenga wilayani humo, vitakidhi mahitaji ya jamii kwani Sera ya afya inataka watu 50,000 wahudumiwe katika kituo kimoja cha afya.  


Imeandikwa na Fred Kibano

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.