• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Sera ya Ugatuaji wa madaraka yaleta mabadiliko

Imewekwa tar.: June 4th, 2018

Na Angela Msimbira, Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amasema kuwa Sera ya Ugatuaji wa madaraka imeongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akitoa maelezo katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa, Utawala na Serikali za Mitaa, na hesabu za Mashirika ya umma kilichoafanyika leo katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Jijini Dodoma.

Amesema kuwa karibu asilimia 90 ya vijiji na kata zinaandaa na kuwasilisha mipango shirikishi kwa wakati na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mipango kwa kutumia mfumo wa fursa za vikwazo katika ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa, Ujenzi wa Zahanati, Vituo vya afya na miradi mingine ya maendeleo.

Mhandisi Iyombe amesema kuwa mpaka sasa Serikali inashule za sekondari za kata zipatazo 3,516 ambazo kwa sehemu kubwa zimejengwa kwa nguvu za wananchi ambapo nguvu hizi zimekuwa zikienda kasi wakati mwingine kutoendana nauwezo wa Serikali wa kuajiri wataalam, vifaa na na fedha za kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa na wananchi.

Anafafanua zaidi kuwa Serikali imeweza kuongeza mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutokana na kuongezeka kwa vyanzo vya mapato, uwekezaji na kuimarika kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na matumizi. Pia mamlaka za Serikali za Mitaa zimeweza kupanga na kupitisha bajeti na kuibua vyanzo vya mapato.

Mhe Iyombe amesema kuwa dhana ya Ugatuaji wamadaraka kwa Umma inahusu kupeleka madaraka ya kisiasa kwa wananchi lengo likiwa ni kuwapa wananchi madaraka kupitia kwa viongozi wao wafanye maamuzi yanayohusu kuwapa wananchi uwezo wa kuamua , kupanga,kutekeleza na kutathmini mipango ya maendeleo kupitia wawakilishi wao, viongozi wa serikali za Mitaa kuanzia ngazi ya Kijiji na baraza la madiwani la Halmashauri.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshighulikia afya Dokta Zainabu Chaula amesema serikali imeweza kuboresha huduma za afya ambapo kwa mwaka 2007 idadi ya vituo vya afya ilikuwa 380 na kata zilikwa 2500 lakini mwaka 2017/2018 idadi ya kata ni 4,420 na vituo vya afya vimeongezeka hadi kufikia 535.

Amesema Serikali imejikita katika Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya afya nchini, kuajiri wataalam wa afya, uboreshaji wa takwimu kwa kutumia mfumo wa kielektroniki (GoTHOMIS), ukokotoaji wa mahitaji halisi ya dawa kwa mfumo mpya na kudhibiti makusanyo ya mapato katika vituo vya huduma pamoja na kuhimiza malipo ya kadi
Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. Tixon Nzunda amesema ugatuaji katika elimu hususani Elimu ya Msingi na baadae Elimu ya Sekondari ulitokana na Tamko la Rais la tarehe 12/02/2008 kuhusu kugatua Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari kutoka iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM).

Aidha amesema ugatuaji wa elimu umewezesha kurahisisha Ongezeko la Wanafunzi wa Elimu za Msingi na Sekondari,Takwimu zinaonekana kuwa idadi ya wanafunzi wa Elimu ya Awali imeongezeka kutoka 851,084 (2009) hadi 1,436,322 (2017); Elimu ya Msingi kutoka wanafunzi 8,313,080 (2009) hadi 8,969,110 (2017); Elimu ya Sekondari kutoka wanafunzi 1,293,691 (2009) hadi 1,565,201 (2017).

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.