• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

RC Simiyu Wasaidieni Vijana Kufikiri Michezo ni Ajira na Biashara

Imewekwa tar.: March 7th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataka Maafisa Michezo na Walimu wa Michezo mkoani humo kuwasaidia Vijana wa Kitanzania kutoka kwenye nadharia ya kufikiri kuwa michezo ni afya, urafiki na  burudani tu ili waanze kufikiri michezo katika mtazamo wa biashara na ajira.

Mtaka ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga semina ya  kuwajengea uwezo Maafisa Michezo, Viongozi wa Vyama na Vilabu vya Michezo, makocha na walimu wa michezo shuleni, kwa lengo la  kuchochea maendeleo ya Michezo Mkoani Simiyu,  ambayo yametolewa na Dkt. Angela Daalmann  na Anja Henke ambao ni  Wataalam wa Michezo kutoka Jimbo la Hannover Nchini Ujerumani.

“Tumeleta mafunzo haya tukiamini kuwa Maafisa Michezo wote ndani ya Mkoa wa Simiyu watakuwa na msaada mkubwa kwenye kuwaandaa vijana wa Kitanzania kutoka kwenye nadharia ya kusema michezo ni afya, michezo ni upendo, michezo ni burudani ; nataka Afisa Michezo akienda kwenye implementation(utekelezaji) vijana wa mkoa wa Simiyu waanze kujenga vichwani mwao kuwa michezo ni ajira, michezo ni biashara” alisema Mtaka.

“Katika Dunia ya leo michezo ni biashara kubwa na ni ajira kubwa ya dunia ndiyo maana hapa mmefundishwa kuhusu miradi, hili suala la michezo ni burudani, michezo ni afya,  michezo ni urafiki na upendo libaki kama jambo la pili” alisisitiza

Ameongeza kuwa Maafisa Michezo pamoja na walimu wa michezo Mkoani Simiyu kupitia michezo ya UMITASHUMTA  na UMISETA wanapaswa kuwatambua watoto/vijana wenye vipaji na kuwaandaa kibiashara ili wajue kuwa vipaji vyao ni ajira zao za baadaye.

Aidha, amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kutangaza utalii na kukuza uchumi kupitia sanaa, michezo na utamaduni na akabainisha kuwa Mkoa umeanza kutekeleza hilo kupitia  uanzishwaji wa Tamasha kubwa la michezo na utamaduni maarufu kama “Simiyu Festival” ambalo linafanyika kila mwaka na kwa mwaka 2018 litafanyika mapema mwezi Julai.

Naye Mtalaam wa Michezo kutoka Jimbo la Hannover Dkt. Angela Daalmann amesema kwamba wamehamasika kutoa mafunzo kwa maafisa, viongozi na walimu wa michezo mkoani Simiyu ikiwa ni mara ya pili sasa, kutokana na utayari wa viongozi na watalaam mkoani humo katika kuleta mapinduzi kwenye sekta ya michezo.

Afisa Michezo wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Emmanuel Athanas amesema mafunzo hayo yataamsha ari na hamasa ya michezo kwa Maafisa Michezo na Walimu wa Michezo mkoani humo na kuwasaidia katika kuibua miradi mbalimbali itakayohusianishwa na michezo (sports projects)  sambamba na kuwatafuta wadau mbalimbali kuwezesha miradi hiyo.

Naye Afisa Michezo wilaya ya Meatu, Bw. Hassan Sengulo amesema mafunzo hayo yamewasaidia kutambua namna sahihi ya kupata fedha kwa ajili ya uendeshaji wa michezo,  hivyo watayatumia kuwaelimisha Walimu wa Michezo na Viongozi wa Vyama na Vilabu  vya Michezo namna ya kutatua changamoto ya ukosefu wa fedha za kuendeshea michezo.

Semina hii ilijumuisha jumla ya washiriki 27 kutoka Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu na baadaye ikafuatiwa na Bonanza la michezo kwa wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi kushiriki mchezo wa riadha,  ambapo wanafunzi walipata nafasi ya kukimbia mbio za mita 100, mita 400 na mita 1500 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda B wakitoa burudani ya ngoma 

ya asili ya kabila la Wasukuma katika Bonanza la Michezo

 lililofanyika katika viwanja vya shule hiyo Machi 06, 2018 Mjini Bariadi.


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.