• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Rais Samia Suluhu Hassan Aagiza Mchakato wa Ajira 6,000 za Walimu

Imewekwa tar.: April 6th, 2021

Na Fred Kibano 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kuajiri walimu 6,000 haraka.kuangalia nafasi za ajira za walimu takribani 6,000 na kutangazwa haraka.

Agizo hilo amelitoa Ikulu ndogo Jijini Dar es Salaam leo wakati akiwaapisha Makatibu wakuu wa Wizara, Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa Taasisi na Idara mbalimbali za serikali hii leo ambapo ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kuajiri walimu wapya 6,000 wanaotokana na walimu walioacha kazi, kufariki na kustaafu ili kuziba pengo la watumishi hao kwenye sekta ya elimu nchini.

Akitoa hotuba yake iliyojaa maagizo ya Serikali kwa viongozi wateule, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya sekta ya Afya na Elimu inayoendelea kujengwa ili ikamilike kwa wakati na wananchi wengi wanufaike na huduma za elimu na huduma za afya.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Ofisi ya Rais TAMISEMI kuendelee na ujenzi wa shule 26 zinazoendelea kujengwa kila mkoa ambazo bajeti yake ipo tayari na kwamba zikamilike kwa wakati na kuanza kazi.

Kwenye sekta ya afya, ameagiza kuendelea kwa ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati lakini pia kuhakikisha vituo vya afya vilivyokamilika vimewekewa dawa na vifaa tiba ili vianze kutoa huduma mara moja na kuondoa kero kwa wananchi.

Agizo jingine ni kuona namna ya kutoa ajira mpya za madaktari kwenye vituo vipya vya afya na hospitali za wilaya nchini ambazo zinatokana na uhaba wa wataalam hao kutokana na kukamilika kwa miundombinu mingi ya afya kwenye Mikoa na Halmashauri pamoja na kuwa bajeti ya mwaka huu ni kuongeza vifaa tiba na dawa.

Kuhusu Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuangalie njia ya kufanya kwa pamoja ili kutengeneza barabara za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa fedha za Halmashauri husika kama zipo na kwamba fedha zitakazotoka hazina kwa ajili ya barabara zipelekwe kwenye barabara nyingine kwenye Halmashauri husika.

Katika Hatua nyingine, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Mikoa na Halmashauri kuacha kuwazuia watu kuandika kero zao kuhusu mambo yanayowasibu kwa kuwaficha baada ya kuandika kwenye mabango kwani njia pekee ni kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Vilevile, amewataka viongozi na watendaji kusimamia makusanyo ya mapato na matumizi yake kwa kutumia kanuni na sheria bila kuwa kera kwa wafanyabiashara.

Mwisho ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuongeza nguvu kwenye usimamizi wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kazi ifanyike kwa ufanisi na kuwa na matokeo chanya lakini pia amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia watanzania bila upendeleo.



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.