• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

OR-TAMISEMI Yafanyia kazi Tafiti za NBS

Imewekwa tar.: March 2nd, 2018

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuanzia mwaka 2015-2018 imetekeleza kwa kiasi kikubwa matokeo ya tafiti iliyofanywa na  Ofisi ya Taifa ya Takwimu “NBS” kupitia Jukwaa la kukusanya na kuchambua Takwimu za Afya na Lishe “NEP” iliyofanyika Mwaka 2005-2015. Akizungumza  Kikao cha kuwasilisha taarifa hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali  za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema matokeo hayo yamejikita katika Mpango kazi wa Wizara hii tangu Serikali ya Awamu ya tano ilivyoingia madarakani.

Aliendelea kusema katika eneo la Miundimbinu ya Afya ambayo imeonekana katika Tafiti kuwa haikidhi mahitaji ya wananchi kwa kutokuwa na huduma muhimu kama vile kuwa na Wodi za Mama na Mtoto, huduma za upasuaji  sambamba na uhaba wa wataalamu wa Afya ambapo kwa sasa Wizara inaendelea na maboresho makubwa katika Sekta ya Afya kwa ujumla wake.

“ Hapo awali tulikuwa na Vituo vya Afya 586 ambavyo  vilivyokuwa vinaweza kutoa huduma za Upasuaji ni vilikuwa 120 tu lakini  hivi sasa tumeweza kukarabati vituo 205 ambavyo vyote vitatoa huduma ya upasuaji, vitakuwa na wodi ya mama na mtoto, vichomea taka, chumba cha kuhiadhia maiti, maabara pamoja na Wataalamu wa Afya” Alisema Jafo.

Hivyo kwa kiasi kikubwa tumetembea kwenye matokeo ya Tafiti hii inayowasilishwa leo na tuna uhakika kwenye Tafiti ijayo matokeo yatakuwa tofauti na yalivyo sasa tunajivunia jitihada hizi na tunawapongeza Ofisi ya  Taifa ya  Takwimu kwa matokeo haya.

Wakati huo huo Mhe. Seleman Jafo amewaagiza Watafiti nchini kuwa waadilifu katika kutafuta na kutoa Takwimu sahihi ili Serakali iweze kujitathmini na kuweka mikakati katika utoaji wa huduma katika jamii na kuleta maendeleo.

Amesema kuwa Takwimu zikiwa sahihi na kuandikwa kwa weledi husaidia katika kuleta maendeleo kwa jamii kwa kupanga bajeti zenye uhalisia kulingana na takwimu zilizotolewa ambazo zinaonyesha mapungufu yaliyopo na jinsi ya kutatua mapungufu hayo.

“Takwimu husaidia kupanga mikakati mbalimbali  ya kuleta maendeleo katika Taifa hivyo ni vyema zikawa sahihi na zinazolinda maslahi mapana ya taifa kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.” Amesema Jafo

Jafo amesema pia kuwa takwimu hii imeipa Wizara muelekeo ya kujipima kulingana na kazi mbalimbali za Afya zinazoendelea kufanyika katika maeneo yote Nchini.

Naye Bi. Ruth Minja Kaimu Meneja wa Takwimu za Mazingira kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) amesema   National Evaluation Platform (NEP) ni  Jukwaa ambalo linakusanya na kuchambua takwimu za afya na Lishe kutoka vyanzo mbalimbali ili kuwezesha Serikali kupata majibu ya kimkakati  ya ushahidi ya kitakwimu katika utekelezaji wa Sera na Programu zote zinazo husu afya ya lishe  ya Mama Mjamzito na Mtoto.

Amesema NEP linajumuisha mkusanyiko wa mbinu mbalimbali za kitakwimu ambazo zinawasaidia wafanya maamuzi kuainisha maswali ya kipaombele na kuyafanyia tathmini.

Aidha amebainisha kuwa Uchambuzi umekusanya taarifa muhimu  ambazo zinasaidia kutambua kuwa ni afua zipi za afya  zinafanya vizuri na kubainisha mapungufu  katika utendaji ili kuweka mbinu  na kubuni njia ya kuboresha huduma ya mama na mtoto katika Lishe.

Kikao  cha kupokea  matokeo ya utafiti wa huduma za afya Nchini iliyowasilishwa na  Jukwaa la kukusanya na kuchambua takwimu za afya na Lishe ( National Evaluation Platform-NEP)  na kusimamiawa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa NBS kimefanyika leo  katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Ndg.Mrisho Mrisho akichangia hoja 

wakati wa Kikao cha Uwasilishaji wa Takwimu za Utoaji wa huduma za Afya ya Msingi.

Kaimu Meneja wa Takwimu za Mazingira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja(Katikati) 

akiwasilisha Salamu za Taasisi hiyo kabla ya kuwasilisha Takwimu za Utoaji wa huduma za Afya ya Msingi.

Katika Picha ya pamoja ni Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Selemani Jafo(mbele Katikati), 

Naibu katibu Mkuu Elimu Tixon Nzunda(mbele kushoto), Kaimu Meneja wa Takwimu za

 Mazingira,NBS Bi.Ruth Minja pamoja na wadau kutoka NEP.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.