• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo

OR TAMISEMI, PS3 Wapongezwa kwa Mifumo

Imewekwa tar.: June 12th, 2018

Emelda Malima mhasibu Mwezeshaji, akitoa msaada wa kitaalam wakati wa mafunzo ya Epicor 10.2, 
yanayo endeshwa na OR TAMISEMI chini ya ufadhili wa mradi wa PS3 jijini Mwanza (Picha na Atley Kuni)

OR TAMISEMI, PS3 Wapongezwa kwa Mifumo

Na Atley Kuni OR TAMISEMI
Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI na Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la Misaada (USAID) zimepongezwa kwa kufadhili na kusimamia utekelezaji wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta ya umma PS3 katika halmashauri 185 nchini.


Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni jijini Mwanza na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa Epicor toleo la 10.2, ambao ni Wahasibu na Waweka hazina kutoka Mikoa ya Mwanza, Tabora, Simiyu, Kagera na Mara.


Wamesema katika muda mfupi ambao wameanza kutumia mifumo mbali mbali ya sekta ya umma ukiwemo mfumo wa Epicor, ambao umekuwa na matoleo yaliyotangulia tija na ufanisi imeongezeka katika halmashauri zao.


Miongoni mwa washiriki hao bwana Hussein Yahya, ambaye ni Mhasibu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, ambaye alisema kuwepo kwa mifumo hii mbali na kuwarahisishia utendaji wao wa kazi inawawezesha kuwahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.


“Mifumo hii imeongeza uwazi, na uwajibikaji na inaturahisishia katika majukumu yetu ya kutoa huduma kwa wananchi,” alieleza.


Bwana Yahya aliitaja mifumo hiyo kuwa ni pamoja na mfumo wa matumizi (Epicor), Mfumo wa mapato (LGRCIS), Mfumo wa Hospitali wa mapato pamoja na utabibu (GoTHomIS), na mfumo wa mipango na bajeti (PlanReP).


Aliongeza kuwa licha ya mkoa wake wa Tabora kutokuwa miongoni mwa mikoa ya Mradi wa PS3, lakini wamefaidika na mradi huo kwa kupatiwa mafunzo ya Epicor.


Naye bwana Deusderit Binamungu, Afisa Manunuzi kutoka Halmashauri ya Musoma alisema kuwa wamefaidika na mafunzo ya mfumo huo na kubaini kuwa mfumo wa Epicor toleo la 10.2 ni wenye kasi na unaowezesha kupatikana kwa taarifa kwa muda muafaka.


Kwa upande wake Rozalina Tarimo Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi kutoka Halmashauri ya Maswa, alisema Mfumo wa Epicor 10.2, ni mzuri kwa kuwa kila mtumiaji wa mfumo atakuwa na namba maalum ya siri hali itakayosaidia kuongeza zaidi usalama wa taarifa na udhibiti wa utoaji taarifa.


“Kuanza kutumika kwa mfumo huu kutasaidia udhibiti wa fedha za umma kutumika kiholela, kabla ya Epicor 10.2 suala la masurufu lilisumbua katika urejeshwaji wake,” alieleza na kuongeza:


“Sheria ya manunuzi namba 7 ya 2011 na marekebisho yake ya 2016, inataka ndani ya siku 14 mtu aliyechukua masurufu awe amerejesha toka siku aliyo maliza kazi, lakini ilikuwa tofauti, ambapo sasa mfumo utakapo anza kutumika, mtumishi hataruhusiwa kuchukua masurufu mapya kabla ya kufanya marejesho ya awali,” alisisitiza.


Mradi wa PS3 ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unalenga kutumia TEHAMA kuboresha uandaaji wa mipango, bajeti na usimamizi wa kifedha kwa kila ngazi ya serikali.


Pia Mradi huo unalenga kuimarisha ufanisi, uwazi na uwajibikaji wa matumizi ya fedha kati ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na vituo vya kutolea huduma, kuelekea katika kuboresha huduma za umma kwa wananchi.

Washiriki wa Mafunzo ya toleo jipya la mfumo wa Epicor 10.2 wakifatilia kwa umakini mafunzo hayo
Hussein Yahaya Mhasibu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakati wa mafunzo ya Epicor 10.2
Mtaalam wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Antidius Anatory akitoa 
maelekezo kwa washikiriki wa mafunzo ya Epicor 10.2 jijini Mwanza

Anaandika. Atley Kuni – OR-TAMISEMI

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.