• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Miradi ya Halmashauri ya Chemba ni kichefuchefu

Imewekwa tar.: December 30th, 2020

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amechefuliwa na kitendo cha ucheleweshwaji wa miradi katika Wilaya ya Chemba huku akimwagiza Mkurugenzi kuhakikisha leo saa nne asubuhi anampelekea maelezo ni kwanini wasichukuliwe hatua kwa uzembe huo.

Hali hiyo ilijitokeza leo wakati alipotembelea Miradi inayotekelezwa kwenye Wilaya hiyo ambapo kwa kiasi kikubwa hakufurahishwa na kasi ya ujenzi wakati maeneo mengine nchini imekamilika licha ya fedha kutolewa kwa wakati.

Waziri Jafo ameitaja miradi hiyo kuwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na bweni moja katika Shule ya Sekondari ya Chemba na Jengo la Utawala la Halmshauri ya wilaya hiyo ambayo hadi sasa haina maendeleo yoyote licha ya kutakiwa iwe imekamilika mwaka huu.

Aidha, alikataa kupokea taarifa kuhusu mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ambayo inaeleza uwepo wa mapungufu ya fedha wakati Serikali imetoa Fedha yote bilioni 1.8 lakini wao wanasema bilioni 1.5.

“Nimezunguka nchi nzima lakini hapa Chemba mna hali mbaya na hiyo inasababishwa na baadhi ya viongozi kutojua changamoto za wananchi maana hapa kuna watoto wanahitaji huduma lakini ninyi hamfanyi kazi na ni dhambi kubwa mnafanya” amesema Mhe. Jafo.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus Mashimba na wakuu wa idara  kuwasilisha  kesho maelezo kuhusu kwa nini wasichukuliwe hatua  kwa uzembe wakutokukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati na uzembe uliokidhiri.

“Chemba ni wazembe na mmecheza na fedha licha ya kwamba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe magufuli  ndio ametoa na hii inatokana na wengi wenu mmekulia kwenye mboga nane na hamjui changamoto za wananchi wa chini,”amesisitiza Waziri Jafo.

Waziri Jafo ameongeza kuwa hawezi kuhangaika kwa watu ambao hawana uchungu na wananchi na kwamba kuna viongozi wamepewa dhamana lakini hawajui matatizo.

Kuhusu ujenzi wa Bweni na shule alisema viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba  hawapo makini na kazi kwani miradi mingi imedorora, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleoya halmashauri hiyo.

“kwa sababu haiwezekani hadi leo hamjakamilisha ujenzi wa shule na bweni  ndio mmeanza msingi kwahiyo nataka maelezo kwanini serikali isifanye jambo kwa uzembe huo, ujenzi hospitali za wilaya wenzenu wamefanya mambo makubwa zaidi ya mliyofanya na sijaridhishwa na mmenipa taarifa ya uongo kwamba mmepokea Bilioni 1.5 badala ya bilioni 1.8 ni kosa kubwa.amesisitiza” Waziri Jafo

katika Kutokana na changamoto hizo, Waziri Jafo amemwagiza Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga kuunda timu maalum ili kuchunguza matumizi ya fedha za miradi katika Wilaya hiyo na kazi hiyo ianze Januari mosi hadi 19 mwakani iwe imekamilika.

“Pia wachunguze nani alifanya uzembe na kwanini ziliingia kule na kurudi serikalini pia wachunguze mahusiano yaliyopo baina ya watendaji na wafanyakazi maana hakuna mahusiano mazuri Chemba ili itafutwe dawa ya kuondoa changamoto hiyo,”Amesisitiza Waziri Jafo


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.