• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Mapato ya ndani ya Halmashauri yafikia asilimia 81

Imewekwa tar.: October 5th, 2018

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Serikali imesema kuwa  mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Sh bilioni 553.39 zimekusanywa kati ya Sh bilioni 687.31 ambazo ni sawa na asilimia 81 ya lengo ambalo halmashauri zote nchini ilijiwekea.

Aidha, Dodoma imeongoza katika ukusanyaji wa mapato kwa upande wa majiji na mikoa ambapo Halmashauri ya Mji Geita ikiwa kinara katika mlinganisho wa kiasilimia kwa Mamlaka zote za Serikali za Mitaa bila ya kujali hadhi huku halmashauri ya Mbinga ikishika mkia.

Akitangaza makusanyo kwa halmashauri zilizofanya vizuri na vibaya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alisema: " TAMISEMI imekuwa ikifuatilia ukusanyaji wa mapato katika halmashauri zake ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri zote nchini.

" Baada ya kumaliza zoezi la usuluhishi wa kibenki takwimu zinaonyesha kwamba kwa mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi 553,390,075,912 zimekusanywa kati ya shilingi 687,306,661,000 ambazo ni sawa na asilimia 81 ya lengo."

Jafo alisema kwa upande wa Majiji, Jiji la Dodoma limekuwa la kwanza kati ya majiji sita likiwa limekusanya Sh bilioni 25.06 kati ya Sh bilioni 19.33 ambayo ni sawa na asilimia 130 ya lengo wakati Jiji la Mbeya limekuwa la mwisho kwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 7.82 kati ya Sh bilioni 11.0, sawa na asilimia 71.

Dar es Salaam ni ya pili ikiwa imekusanya Sh bilioni 15.67 kati ya makisio ya Sh bilioni 16.41 ambayo ni asilimia 95, Arusha ya tatu ikikusanya Sh bilioni 13.59 kati ya lengo la Sh bilioni 14.58, Mwanza imeshika nafasi ya nne ikikusanya Sh bilioni 10.47 kati ya malengo ya Sh bilioni 1.44, Tanga ikikusanya Sh bilioni 10.84 kati ya malengo ya Sh bilioni 14.03.

Jafo alisema Manispaa ya Iringa ndiyo ilikuwa ya kwanza kwa kukusanya Sh bilioni 4.28  kati ya Sh 4.17 ambayo sawa na asilimia 103 ikifuatiwa na Manispaa ya Temeke iliyokusanya Sh bilioni 29.41 kati ya lengo la kukusanya Sh bilioni 29.07 sawa na asilimia 101.

Alisema katika kundi hili, Manispaa ya Ilemela ilikuwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 4.76  kati ya lengo la kukusanya Sh bilioni 11.75 sawa na asilimia 40.

Jafo alisema Halmashauri ya Mji wa Geita ndiyo ilikuwa ya kwanza kwa kukusanya Sh bilioni 6.86 kati ya lengo la kukusanya Sh bilioni 3.15 sawa na asilimia 218 ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe iliyokusanya Sh bilioni  2.93 kati ya lengo la kukusanya Sh bilioni 2.40 sawa na asilimia 122.

Alisema Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ni ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 1.14 kati ya lengo la kukusanya Sh bilioni 2.11 sawa na asilimia 54.

Jafo alisema Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ilikuwa kinara kwa kukusanya Sh bilioni 3.09 kati ya Sh bilioni 1.87 sawa na asilimia 165 ikifuatiwa na Halmashauri ya Mpimbwe iliyokusanya Sh bilioni 1. 55 kati ya Sh milioni 956.84 sawa na asilimia 162.

Alisema halmashauri za wilaya zilizofanya vibaya zaidi ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyokusanya asilimia 20, halmashauri ya Songea iliyokusanya asilimia 33, Halmashauri ya Rorya ilikusanya asilimia 37 na Halmashauri ya Siha iliyokusanya asilimia 39.

Aidha, Jafo alisema katika mlinganisho wa kiasilimia kwa Mamlaka zote za Serikali za Mitaa bila ya kujali hadhi zao, halmashauri tatu kinara kwa makusanyo kiasilimia ni Halmashauri ya Mji wa Geita ambayo imekusanya kwa asilimia 218, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ambayo imekusanya kwa asilimia 165 na Halmashauri ya Mpimbwe iliyokusanya kwa asilimia 162 .

" Vivyo hivyo, Hamashauri tatu ambazo zimekusanya kwa asilimia ndogo zaidi ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyokusanya kwa asilimia 20, Halmashauri ya Wilaya ya Songea asilimia 33 na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya iliyokusanya kwa asilimia 37."

Jafo alisema kwa mwaka wa fedha 2017/2018,  halmashauri 38 sawa na asilimia 24 ya Halmashauri zote nchini ziliweza kuvuka malengo yake ya mwaka ambazo ni  Geita TC, Kibaha DC, Mpimbwe DC, Kaliua DC, Misungwi DC, Bukoba DC, Pangani DC, Kilindi DC, Kilombero DC, Kibondo DC, Makete DC, Dodoma CC, Wanging'ombe DC, Longido DC, Ulanga DC, Kasulu DC, Bukombe, Njombe TC, Ushetu DC, Handeni TC, Mpanda DC, Muleba DC, Babati DC, Mwanga DC, Kibaha TC, Bunda TC, Mbozi DC, Ukerewe DC, Tandahimba DC, Magu DC, Newala DC, Monduli, Malinyi DC, Lushoto DC, Njombe DC, Iringa MC, Tarime DC, na Temeke MC

Pia halmashauri 14 sawa na asilimia 7.57 hazikuweza kufikia asilimia 50 ya malengo yake ambazo ni  Iringa DC, Kyerwa DC, Mbulu DC, Kishapu DC, Igunga DC, Chato DC, Itilima DC, Itigi DC, Ubungo MC, Ilemela MC, Siha DC, Rorya DC, Songea  DC, na Mbinga DC

Jafo alisema mamlaka nne ziliibuka kinara kwa kukusanya mapato mengi ambazo ni Manispaa ya Ilala (Sh bilioni 44.51), Kinondoni (Sh bilioni 29.75), Temeke (Sh bilioni 29.41) na Dodoma ilikusanya Sh bilioni 25.06.

Alisema pia halmashauri tatu zilizokusanya mapato kidogo bila kujalisha asilimia ya makusanyo yao ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko (Sh milioni 347.15), Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe (Sh milioni 37.22) na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (Sh milioni 418.79).

Jafo alisema halmashauri za mikoa mitatu ziliifanya Mikoa yao kuwa kinara kwa makusanyo ya mapato ya ndani ambayo imeongozwa na Dodoma iliyokusanya kwa asilimia 170, Geita imekusanya kwa asilimia 104 na Njombe uliokusanya kwa asilimia 103.

" Mikoa hii mitatu ndiyo iliyovuka malengo yake katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka uliopita.".

Jafo alisema mikoa mitatu ambayo ilikusanya kwa asilimia ndogo ni pamoja na Ruvuma uliokusanya kwa asilimia 46, Simiyu asilimia 59 na Shinyanga asilimia 66.

Akizungumzia mikakati ya uamarishaji wa makusanyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Jafo aliziagiza halmashauri zote zilizokusanya chini ya asilimia 50 ya lengo kwa mwaka uliopita zimetakiwa  kutoa maelezo ni kwanini hazikufikia hata asilimia 50 ya lengo walilojiwekea.

" Nawaelekeza Wakuu wa Mikoa kufuatilia ufujaji wa mapato katika Halmashauri zilizopo kwenye Mikoa yenu ili kubaini wanaohusika kufanya uzembe wa aina yoyote uliojitokeza katika ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri hizo ili endapo itabainika kulikuwa na hujuma ya makusudi kwenye ukusanyaji chukueni hatua za kinidhamu na kisheria.

Aliongeza: " kwasababu wastani wa makusanyo ni asilimia 81, basi hii itakuwa ndio kiwango chetu cha chini, hivyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ni kila Halmashauri katika Mikoa yote isikusanye chini ya asilimia 81 ya lengo lake.  Hivyo, Wakuu wa Mikoa mnapaswa kusimamia mkakati huu katika Mikoa yenu.

Pia Jafo aliwataka wakuu wa mikoa kusimamia halmashauri zao ili kudhibiti matumizi ya mapato ya ndani yanayokusanywa kwa lengo la kufanikisha Miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Aidha, Jafo alisema wakurugenzi watapimwa utendaji wao kwa kuangalia suala la utekelezaji wa mapato kwa mwaka 2018/19.

" Kwa mwaka 2018/2019, pia tutaangalia suala la makusanyo na matumizi, maana kukusanya ni jambo jingine na kutumia ni jambo jingine, hivyo tuanaangalia katika kilichokusanywa ni kiasi gani kimepelekwa kutekeleza miradi ya maendeleo."

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mhandisi Mussa Iyombe alisema pamoja na kufuatilia kwa karibu halmashauri ambazo zimefanya vibaya katika ukusanyaji mapato, lakini pia itaziangalia zile ambazo zingeweza kukusanya maradufu ya lengo ili kuangalia kama ziliweka makisio ya chini ili baadae zionekane zinafanya vizuri.

" Katika hili hatutamuonea mtu, na hata hatutamfumbia macho mtu yeyote ambaye ameshindwa kuwajibika katika nafasi yake, lakini tutaziangalia hata zile halmashauri ambazo uchumi wake ni mzuri lakini kwenye makusanyo hazikufanya vizuri sambamba na zile ambazo zimeweka makisio ya chini," alisema.

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.