• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Majaliwa awataka Mkalama kutumia fursa ya daraja la Msingi Lukomo

Imewekwa tar.: July 18th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa Kata za Iguguno, Ntonda, Kiyangire na Wilaya ya Mkalama kutumia fursa ya daraja la Msingi lililopo Lukomo na barabara zilizojengwa na TARURA kusafirisha mazao na biashara zao ili kuendelea kujikwamua kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa Wilayani Mkalama wakati akikagua ujenzi wa daraja la Lukomo barabara ya Iguguno-Kikhonda-Kinampanda lenye urefu wa mita 30 ambalo limekamilika kwa asilimia 100 mapema ambapo amewataka wananchi kulitumia kama fursa ya kiuchumi kwani linaunganisha Kata za Wilaya hiyo na mkoa wa Simiyu.

“andaeni biashara zenu, tumieni fursa ya daraja na barabara zilizojengwa kupitisha biashara zenu, ubora wa daraja hili ni ubora wa kudumu, niwapongeze sana Wahandisi wa TARURA mkoa wa Singida, huu ni ubunifu wa kujenga daraja kwa shilingi milioni 550 badala ya shilingi Bilioni moja iliyotakiwa itumike” alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itafanya kazi usiku na mchana kuwatumikia wananchi ili kuhakikisha inafikia malengo.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David amesema daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 550 na litakuwa na uwezo wa kupitisha magari ya mizigo yaliyobeba mpaka tani elfu 40 na litasaidia kuokoa maisha ya watu yaliyokuwa yakipotea karibu kila mwaka kwa  takribani miaka 40.

“daraja hili limejengwa kwa kutumia mawe na nondo na limetumia muda mfupi kukamilika, kutoa ajirra kwa maeneo huisika,  kukamilika kwa ujenzi huu wa daraja kutaondoa changamoto ya mawasiliano iliyokuwepo hasa kipindi cha masika, aidha kutaimarisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Kata za Iguguno, Kikhonda na Kiyangire”

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (AFYA) Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imekubaliana na Mameneja wa TARURA kuwa wabunifu na kuhakikisha barabara wanazosimamia zinapitika kwa kipindi cha mwaka mzima. Ameishukuru Serikali kuongeza bajeti ya barabara kupitia Wakala wa Barabara TARURA kutoka shilingi Bilioni sita hadi shilingi Bilioni 23.4 kwa mwaka mkoani Singida sawa na ongezeko la asilimia 389 na shilingi milioni 600 hadi shilingi Bilioni 2.2 kwa Halmashauri ya Mkalama.

Kwa upande wake Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Isack Mtinga amesema Serikali imefanya jambo kubwa kujenga daraja la Lukomo na lakini ameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Lukomo ili ianze kutoa huduma.

Naye Mzee Omari Ngaa mwenyeji wa eneo la Lukomo - Iguguno amesema tangu akiwa kijana mdogo eneo hilo huwa mto mkubwa kipindi cha masika na kipindi cha kiangazi haukauki na kabla ya daraja halijajengwa watu zaidi ya 15 walipoteza maisha.

“daraja hili ni zuri sana, ninaishukuru sana Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan mimi toka nikiwa mdogo nimeshuhudia watu zaidi ya 15 wakichukuliwa na maji na kufa, daraja hili litatusaidia usafiri kwani mwanzo usafiri ulikuwa wa tabu sana”


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.