• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo

Serikali yaanza kuandaa Mpango rasmi wa kukabiliana na uhaba wa watumishi

Imewekwa tar.: February 1st, 2022

Na Fred Kibano, Morogoro

Serikali imesema mafunzo juu ya orodha na maelezo ya kazi yatawezesha Mpango wa Serikali wa kupunguza uhaba wa watumishi Serikalini ambao unatokana na kutobainishwa kisayansi bila ya kuangalia uzito wa majukumu ya watumishi kwenye Taasisi za Serikali.

Akifunguzi mafunzo hayo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Morogoro hivi leo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema uhaba wa watumishi Serikalini kwa sehemu kubwa unatokana na kutobainishwa kisayansi bila ya kuangalia uzito wa majukumu ya watumishi katika Tasisi za Serikali na ndiyo maana Mifumo ya kiutawala imekuwa ikiandaliwa na kutumika kukabiliana na uhaba huo.

Dkt. Ndumbaro amesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikiweka Mifumo mbalimbali ya kimenejimenti ili kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku na hivyo zoezi hilo la kuandaa orodha ya kazi kwa wakati huu ni muhimu kwa kila Taasisi ya Serikali.

“Orodha ya kazi ni Mfumo wa Kimenejimenti unaowezesha kuainisha mahitaji kwa idadi na aina ya watumishi, cheo na majukumu yote yanayopaswa kutekelezwa kwa kila mtumishi katika kila cheo kwa mujibu wa muundo na mgawanyo wa majukumu ya Ofisi” alisema Dkt. Ndumbaro.

Aidha, amesema lengo sio kuwapunguza watumishi wa Umma bali ni kuangalia uhaba na upungufu mkubwa wa watumishi kwenye kada mbalimbali na kuweza kupunguza upungufu uliopo kabla ya kuajiri watumishi wengine ili kuboresha utendaji kazi wa shughuli za Serikali katika ngazi zote.

“hii itasaidia kubaini maeneo ambayo yanaupungufu mkubwa wa watumishi kuwa ni kiasi fulani na utoshelevu ni kiasi fulani ili tuweze kuwaondoa wengine kwenye maeneo ambayo wamezidi na kuwapeleka kwenye maeneo ambayo yanakabiliwa na upungufu mkubwa kabla ya kuajiri watumishi wapya” alisema Dkt. Ndumbaro.

Akitoa maelezo ya awali kwa niaba ya katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof. Rizikiki Shemdoe kabla ya hotuba ya mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mariam Ntunguja amesema mafunzo hayo yataleta tija kuanzia Ofisi ya Rais TAMISEMI Makao Makuu, Mikoa, Halmashauri na Tasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“baada ya kukamilika kwa mafunzo haya kazi inayofuata ni kuandaa mahitaji ya watumishi kwenye ngazi ya Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa” alisema Ntunguja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Bwana Marko Masaya amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI inaundwa na vitengo 6 na idara 11 ambapo idadi ya watumishi waliopo makao makuu ni 520 lakini pia kikosi kazi hicho kinawajumbe wapatao 32 hivyo zoezi la kuandaa orodha ya kazi na maelezo yake itasaidia kujua idadi ya watumishi kwa kuzingatia mahitaji halisi ya watumishi kwa kuzingatia muundo wa wizara.

Mwenyekiti wa kikao kazi hicho Bwana Boniface Luhende akiongea kwa niaba ya wajumbe wenzake amesema tangu mafunzo hayo yalipoanza yamekuwa na mafanikio na kwamba wataendelea kupokea maelekezo mbalimbali na kuyafanyia kazi ili kufanikisha azma ya kikao kazi hicho.



Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.