• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Kahama yajipanga Kufikia Tanzania ya Viwanda

Imewekwa tar.: February 17th, 2020

Serikali imepongeza hatua ya halmashauri ya Mji Kahama kutenga eneo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na kuwamilikisha hati za viwanja ili kuwainua wananchi hao kiuchumi.

Mhandisi Joseph Nyamhanga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara yake ya kikazi  kukagua miradi ya maendeleo na kuona utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni pamoja na eneo lililotengwa na halmashauri ya Mji Kahama.

Mhandisi Nyamhanga alisema kutenga eneo kubwa na la kutosha kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara wakubwa ni dhahiri halmashauri inaunga mkono  Serikali ambayo imeamua kuingia katika Tanzania ya viwanda kwa kuwawezesha wananchi wake kiuchumi na hilo ndilo lengo la nchi.

Aidha, alitoa rai kwa ofisi za Umma wilayani Kahama kununua bidhaa bidhaa za wajasiriamali hao ili kuwainua kiuchumi na kuwajengea uwezo kifedha pamoja na kujiajiri.

Alisema asilimia 10 inayopaswa kutengwa kwa ajili ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu ni jukumu la kila halmashauri kuyabaini makundi haya na kuwapatia mikopo lakini kuhakikisha manarejesho yote ya mikopo yanatekelezwa katika muda uliopangwa ili wengine nao waweze kukopa.

Nyamhanga alisema Sambamba na makundi hayo kufanya biashara na kujiajiri itaongeza mapato ya halmashauri husika na mapato ya Serikali Kuu kwa ujumla.

Aidha, aliuagiza Wakala wa Barabara ‘TARURA’ kujenga barabara inayoelekea katika eneo la viwanda lililotengwa kwa ajili ya wawekezaji wadogo na wakubwa ili kuondoa changamoto ya baadhi ya magari makubwa kushindwa kupita na kushusha mizigo mikubwa.

Anamringi Macha Mkuu wa Wilaya Kahama alisema haikuwa kazi rahisi kuwashawishi na kuwaunganisha vijana na kasha kuwahamisha kutoka katikati ya Mji wa Kahama lakini pia walitatua changamoto ya fedha kwa kuwapatia mkopo wa shilingi milioni 100 na pia kuto na kuwatafutia masoko kwa kutoa rai kwa ofisi zote za Serikali wilayani Kahama kununua samani za ofisi kutoka Y- Times furnature (kiwanda kidogo) lakini pia Taasisi za Serikali zainazohusiana na viwanda zimekaribishwa kuwekeza kwenye eneo la viwanda  ili kuwafundisha vijana na wajasiriamali wengine namna ya kuongeza thamani  ya bidhaa zao na kushindana sokoni.

Richard Sabi kijana mjasiriamali anayemiliki kiwanda cha samani amesema walianza na mtaji mdogo lakini kwa sasa wamekwisha fikisha kiasi cha shilingi milioni 200 baada ya kupata mkopo wa shilingi milioni 100 na kuzalisha. Aidha, alizitaja baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa kiwandani hapo kuwa ni pamoja na milango, vitanda, sofa, meza na vitu vingine.  

Mhandisi Nyamhanga pia alitembelea shule ya sekondari Mwakata iliyopo halmashauri ya wilaya Msalala na kituo cha afya Tinde kilichopo halmashauri ya wialaya ya Shinyanga ambapo aliwaasa Viongozi wa wilaya hizo kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi ya sekta zote zikiwemo elimu na afya, kufanya kazi kwa weledi lakini pia kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali.

                  Anaandika Fred Kibano

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.