• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Jafo agoma kuiongezea shilingi milioni 200 Halmashauri ya Jiji la Dodoma

Imewekwa tar.: November 4th, 2019

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amekataa kuiongezea Halmashauri ya Jiji Dodoma kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa shule ya mfano na kuagiza kuwa ujenzi wa shule hiyo uwe umekamilika ifikapo Novemba 30 mwaka huu.

Ameyasema hayo leo kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi ya mfano inayojengwa katika Kata ya Ipagala, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mhe. Jafo ametoa   msimamo huo baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo na kuwa bado zinahitajika takribani sh milioni 241.931 ili kukamilisha ujenzi huo.

 “Inanipa tabu kuelewa kuwa ujenzi huu haujakamilika na mnataka fedha zaidi wakati mlipewa kiasi cha shilingi 706,400,000 na wezenu kupitia fedha hizo wameweza kukamilisha ujenzi na tayali shule zimeanza kufanya kazi” Amesema Mhe. Jafo

Mhe. Jafo ameutaka uongozi wa Jiji hilo kutafuta  fedha sehemu nyingine ili kukamilisha ujenzi  wa shule hiyo ya mfano na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa muda unaotakiwa kwa kuwa Serikali hapo tayari  kuongeza fedha ili kukamilisha ujenzi huo

“Naomba niwaeleze kwamba hiyo fedha shilingi milioni 200 haitaweza kupatikana kutoka ofisini kwangu, lakini hata mkitoa kwenye vyanzo vya ndani ni kujitia hasara isiyokuwa na sababu kwani kama mliona gharama ya ujenzi ni kubwa mlitakiwa kuona, hata mkajenga madarasa 12 kati ya hayo 17 lakini yawe yamekamilika kuliko hali ilivyo sasa, inamaana bila kuongeza hizo fedha mradi huu hautaisha” Amesisitiza Mhe. Jafo.

Aidha Mhe. Jafo ametoa wito kwa Hamashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha wanasimamia ujenzi  kikamilifu  ili kuweza kukamilika kwa muda unao takiwa na ujenzi huu kuwa katika ubora unaoendana na kiasi cha fedha kilichotolewa  na Serikali.

Akitoa taarifa, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la  Dodoma Bw. Charles Mabeho amesema  awali walipokea sh milioni 706.4 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na kuwa mpaka sasa tayari zimetumika shilingi  milioni 677.4 na kubakiwa na shilingi  milioni 29, fedha ambazo hazitaweza kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amekiri kuwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma umeteleza katika utekelezaji wa ujenzi huo ila kupitia muda waliyopewa watajipanga vyema kuhakikisha ujenzi huo unakamilika katika ubora unaohitajika na kuendana na gharama za fedha zilizotolewa na Serikali.

" Hii ni sawa na mradi wa hospitali ya Uhuru, makadilio yalikuwa ni kujenga kwa sh bilioni 6, na Rais ametoa Shilingi bilioni 3.4 na baada ya kukubaliana mapema wataalamu walikaa na kupanga upya na sasa inajengwa kwa fedha iliyopo, hivyo tunaomba radhi." Amesema Mhe. Mahenge

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw.  Godwin Kunambi amesema ofisi yake itaangalia namna ya kutoa fedha hizo katika mapato ya ndani ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

"Kwenye bajeti yetu tuna mapato ya ndani takribani shilingi bilioni 8, hivyo tutatoa kiasi hicho kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo”. Amesisitiza Kunambi

Aidha, Jafo amewaagiza kuhakikisha ifikapo Novemba 30 shule hiyo iwe inekamilika na kuhakikisha wameiweka katika mazingira ya wanafunzi kujifunza.

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI





Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA ATNO AWAMU YA PILI,2023 September 27, 2023
  • TANGAZO LA KUTWA KAZINI September 13, 2023
  • Terms of Reference TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS PROJECT (TACTIC) September 01, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA MPYA 2023 AWAMU YA PILI August 30, 2023
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KWA SHULE MPYA ZA SEKONDARI,2023 August 25, 2023
  • KUSIMAMISHWA KAZI KWA MKURUGENZI WA BUHIGWE July 12, 2023
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • DMDP II MBIONI KUANZA KAZI ZA UJENZI

    September 27, 2023
  • SHULE SALAMA MWAROBAINI WA UKATILI DHIDI YA WATOTO

    September 27, 2023
  • NDEJEMBI ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATAALAM WA ELIMU

    September 18, 2023
  • DKT. SAMIA ASHANGAZWA NA HALMASHAURI KUSHINDWA KUJENGA JENGO LA X-RAY

    September 17, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.