• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
    • Machaguo Kidato cha 5 & Vyuo

JAFO AAGIZA UJENZI WA HOSPITAL YA UHURU UANZE MARA MOJA

Imewekwa tar.: June 19th, 2019

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) ameagiza ujenzi wa Hospital ya Uhuru uanze Wiki ijayo Tar.24/06/2019 ili kutimizia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Dec, 2018 na kuelekeza fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Waziri Jafo alitoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani Chamwino kukagua ujenzi wa hospital hiyo ya kisasa na  kukuta  hakuna ujenzi ulioanza na hata eneo  hilo halijasafishwa.

Akizungumza katika ziara hiyo Jafo amesema hataki kusikia hadithi zozote zinazokwamisha kuanza kwa ujenzi wa Hospital ya Uhuru kwa sababu Agizo lilishatoka na fedha zilishatengwa.

“Sikutarajia kukuta eneo la ujenzi likiwa katika hali hii, hakuna kitu kilichofanyika mpaka leo halafu mnaniambia bado mnaendelea na vikao sijui mnajadili nini ambacho hakiishi ninachotaka kuona hapa ni ujenzi kuanza mara moja yaani ikifika Jumatatu hali ya hapa iwe tofauti mkamilishe mambo yote yanayotakiwa kwa siku hizi chache na kazi hii ianze”

Waziri Jafo aliongeza kuwa nimesikia bado mnajadili kuhusu ramani gani itumike katika ujenzi huu sasa naagiza ujenzi wa Hospital hii utumie ramani ya Hospital ya Tunduma ambayo ni Gorofa kwa sababu ramani ile  itasaidia katika matumizi bora ya Ardhi na pia itakidhi mahitaji ya kuwa na jengo la kisasa lenye hadhi ya Hospital ya Uhuru.

Wakati huo huo Waziri Jafo aliagiza  kikosi maalumu cha SUMA JKT kitumike katika ujenzi wa hospital ya Uhuru ili iweze kwenda na muda na  ubora uweze kuzingatiwa na Wakala wa Majengo (TBA) watumike kama washauri na wadhibiti Ubora wa Majengo ya Hospital hiyo.

“Natoa miezi sita ujenzi wa Hospital hii uwe umekamilika na  ndio maana nikaagiza Kikosi cha Jeshi SUMAJKT  kitumike  ili tuweze kwenda na muda kwahiyo ifikapo Dec, 2019 nataka kuja kuona majengo yote  ya Hospiatl yakiwa yamekamika na kwa ubora wa hali ya juu” Alisema Jafo.

Akitaja sababu zilizochelewesha ujenzi wa Hospital ya Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belnith Mahenge amesem  michoro ya Hospital imechelewa kupatikana na zaidi fedha zilizoelekezwa hazijaingia kwenye Akaunti husika ili ziweze kutumika kwenye  ujenzi.

Aidha Rc Mahenge  ameshkuru Waziri Jafo kwa ziara yake na kusema maagizo yote yaliyotolewa yamepokelewa  na yatatekelezwa; Ujenzi wa Hospital ya Uhuru  utaanza mara moja.

Ujenzi wa Hospital ya Uhuru ni Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa mwezi Dec, 2018 ambapo aliagiza shilingi bil. 900  zilizokuwa zitumike kwenye  sherehe za maadhimisho ya Uhuru  wa Tanzania zitumike kujenga Hospital Kisasa Mkoani Dodoma na  kuongezafedha zaidi shilingi  Bil 2.5 kutoka katika Gawiwo lililotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • TANGAZO LA KAZI - TOA July 22, 2022
  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Utekelezaji wa Miradi ya Elimu isimamiwe na kukamilika kwa wakati- Dkt. Msonde

    August 15, 2022
  • UBUNIFU KIVUTIO UMISSETA 2022

    August 15, 2022
  • Bilioni 776.6 zaelekezwa katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara vijijini na mijini katika mwaka wa fedha 2022/23

    August 14, 2022
  • TARURA KUONGEZA MTANDAO WA BARABARA ZA LAMI KM 1,450, CHANGARAWE KM 73,242’ ENG. SEFF

    August 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.