• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo

Hospitali 67 za Wilaya Kuongezewa Milioni 500 Baada ya Tathmini

Imewekwa tar.: September 14th, 2019

Serikali imesema itaongeza fedha za ujenzi wa hospitali za Wilaya zipatazo 67 zinazojengwa nchini kote baada ya kufanya tathmini ya kina kubaini sababu za kushindwa kukamilisha hospitali hizo.

Akiongea katika hospitali ya kwanza ya wilaya wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Longido leo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI ilikwishatoa mwongozo wa ujenzi kwa kutumia mafundi wazalendo (Local Fundi) au taasisi za kitanzania ambazo zina gharama nafuu lakini pia kutumia sheria za manunuzi ya Umma ili kuepuka hoja za ukaguzi na kuzingatia thamani halisi ya fedha.

Mhandisi Nyamhanga amesema kiasi cha shilingi Bilioni moja na nusu zilizotolewa awali zilikuwa zimalize majengo yote saba lakini pamoja na kuwa sasa zimetengwa shilingi milioni 500 kwa hospitali hizo ili kumalizia baadhi ya gharama zilizoongezeka kutokana na sababu mbalimbali, ofisi yake itafanya tathmini ya kina kujiridhisha na sababu za kutokukamilika kwa baadhi ya hospitali na fedha zote kutumika.

Aidha, amesema kuwa jumla ya hospitali 27 nyingine mpya zinatarajiwa kujengwa katika halmashauri mbalimbali ili kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.

Amewataka watendaji kusimamia utoaji wa huduma bora za afya ili ziendane sambamba na ujenzi wa miundombinu ya hospitali zote.

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega amesema mkoa wa Arusha umepata fedha za ujenzi wa hospitali 4 za wialya na kwa wilaya ya Longido ni hospitali pekee ya kwanza kujengwa tangu Uhuru.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Longido Dkt. Justice Munisi amesema mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 63 kwa majengo yote yaliyokwishajengwa ambayo ni jengo la wagonjwa wan je (OPD), jengo la mionzi, maabara, wodi ya mama na mtoto, bohari ya dawa, jengo la kufulia na wodi ya wazazi.

Wakati huo huo Mhandisi Nyamhanga amekagua kikundi cha akina mama cha Blessings Longido kinachojishughulisha na utengenezaji wa mikate na kimepokea mkopo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Longido shilingi milioni 10 kama ilivyoamriwa kwa halmashauri zote kutenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani ambapo asilimia 4 wanawake, 4 vijana na 2 walemavu. Kikundi kingine alichokitembelea ni Tumaini Osiligi cha walemavu kinachojihusisha na ufugaji wa mbuzi na ununuzi wa mazao.

Pia amekagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita0.8 kuanzia kituo cha polisi hadi shule ya msingi Longido inayogharimu shilingi 248,770,000 chini ya mkandarasi M/S Meero Contractors Co Ltd ya Jijini Arusha ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 98.

Afisa Maendeleo ya Jamii Longido Bi. Grace Mgase amesema kuna jumla ya vikundi 43 ambapo 23 ni vya wanawake na mpaka sasa halmashauri imekwishatoa shilingi 132 milioni zaidi ya lengo lililowekwa la kutoa shilingi milioni 110.

       Anaandika Fred Kibano

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.