• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Halmashauri Nchini zapokea Magari 50 ya Wagonjwa.

Imewekwa tar.: March 20th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, ameendesha zoezi la kugawa magari 50 ya  wagonjwa aina ya Suzuki Maruti (Ambulances) kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Magari hayo ambayo awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliagiza yafanyiwe utaratibu wa kisheria wa kiforodha na  yagawanywe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili yatumike kwa kuwahudumia wananchi katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

“Hii ni agenda ya Mhe. Rais ya kutaka kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora, ambulance hizi ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana na zitatusaidia katika halmashauri nyingi”

Mhe. Jafo amemshukuru Mhe. Rais kwa kuonyesha mapenzi makubwa  lakini pia amependezwa na Watumishi wa Wizara, Mikoa na Halmashauri zote kuweza kuhudhuria hafla hiyo muhimu iliyofanyika katika eneo la bandarini Jijini Dar es Salaam.  

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula amemshukuru Waziri wa Nchi na Waheshimiwa Wabunge kwa utendaji wao na kuwaomba wabunge kuwa na lugha ya ufahamu unaoafanana ili kuboresha utendaji wa Serikalini.

“kwa niaba ya watendaji nawashukuru sana waheshimiwa Wabunge, nilitamani tutembee pamoja kwa maana ya kuwa na uelewa wa pamoja  na ndio maana Mhe. Waziri amewakabidhi wabunge magari nao watukabidhi sisi”

Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Charles Kichere, amesema awali magari hayo aliyaona Mhe. Rais alipofanya ziara bandarini na kwamba magari hayo yalikuwa yameteleekezwa na wamiliki wake kutofahamika na ndipo aliagiza kufuata utaratibu wa forodha na kuyataifisha magari hayo na kisha yagawiwe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Kwa upande wake Mhe. Prof Norman Sigalla King, Mbunge wa Makete, amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa ambulance hizo kwa ajili ya kuimarisha huduma za mama wajawazito.

“kwanza nitoe shukrani za pekee kabisa kwa kupewa ambulance kwa ajili ya wilaya yangu ya Makete nakumbuka niliomba kwa ajili ya tarafa za Ukutama, Matamba, Magomba, Tulongwa na Niwaho” amesema umbali wa kata ya Ukutama hadi Makete mjini ni kilomita 70 na hivyo itawanusuru wakina mama dhidi ya vifo vya uzazi visivyotarajiwa.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Hakimu Ndatama amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia ambulance ambayo itaokoa vifo vya akina mama na watoto kwa kiasi kikubwa.

Kutolewa kwa magari hayo kwa Mamalaka za Serikali za Mitaa ni sehemu ya kuimarisha huduma za afya nchini.

                    Baadhi ya magari aina ya Suzuki Maruti ambayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli 

                      aliamuru yagawiwe katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuhudumia Sekta ya Afya nchini

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.