• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali Yataka Matokeo Chanya Mfumo wa Ugavi na Usambazaji Dawa

Imewekwa tar.: September 11th, 2018

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI), Mhandisi Mussa Iyombe, amewataka wadau wa afya wanaofanya kazi chini ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kufuata utaratibu uliowekwa katika kutekeleza majukumu yao.

Mhandisi Iyombe ameyasema hayo leo jijini Dodoma, wakati akifungua kikao cha siku moja kilichowakutanisha Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Wadau mbalimbali wa afya (eneo la Mfumo wa Ugavi na Usambazaji Dawa nchini) pamoja na Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI.

Amewataka Wadau hao kuwa na malengo yanayoendana na OR - TAMISEMI, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana, kukaa pamoja na kupanga mikakati ambayo itatoa mwelelekeo ambao utampa kila mmoja dira ya majukumu yake ili kuepuka muingiliano wa kazi .

Amesema lengo la kuishirikisha Ofisi ya Rais - TAMISEMI ni kufanya kazi zenye ufanisi zitakazoleta matokeo chanya kwa wananchi na kuepuka kurudia kufanya makosa kama yaliyotokea hapo awali ambapo fedha nyingi za wafadhili zilipotea pasipokuwa na matokeo chanya.

“Kuna wakati unakuta Wadau wanafanya kazi fulani, na sisi tunafanya kazi hiyo hiyo, tunapaswa tugawane cha kufanya ili wananchi wapate huduma bora, tumekaa miaka mingi, tumetoa pesa nyingi, lakini wananchi hawaoni matokeo yoyote, tuna mikakati mizuri lakini hakuna matokeo chanya” Alisema Mhandisi Mussa Iyombe.

Hata hivyo, Katibu Mkuu Mhandisi Iyombe alimtaka Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula kukaa na Wadau hao mara kwa mara kwa lengo la kuwapa miongozo wa nini kinatakiwa kufanyika ili kuacha kurudia makosa yaleyale kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande wake Dkt. Zainab Chaula amewataka Wadau hao wa afya kufanya kazi kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo inatoa dira ya nini serikali inataka kifanywe, kwa kuzingatia pia suala la afya ni kipaumbele namba moja katika Ilani hiyo.

“Tumeitana hapa ili tutembee pamoja, tufanye kazi kwa utaratibu uliowekwa, ili wananchi wapate mabadiliko waliyoyataka, Ilani ndiyo nyenzo ya kufanyia kazi, kila mmoja atembee nayo aisome, Serikali inafanya kazi na kila mdau lakini kwa kufuata utaratibu uliowekwa” Alisisitiza Dkt. Chaula.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Afya Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Wadau hao wa Mfumo wa Ugavi na Usambazaji dawa katika Sekta ya afya wamekubaliana kutekeleza mambo muhimu ya afya ambayo Serikali imeyapa kipaumbele ili kuboresha afya ya Watanzania.


     Anaandika Zulfa Mfinanga na Magdalena Dyauli

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.