• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali yaendelea kuboresha mfumo wa huduma kwa wateja katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Imewekwa tar.: June 30th, 2020

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia maswala ya Afya, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa watumiaji wa huduma za afya nchini katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za halmashauri kutumia namba za huduma kwa wateja zilizopo katika vituo hivyo ili kuwasilisha kero zao mahali sahihi na kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Ametoa wito huo  huo leo Jijini Dar es Salaama  kwenye  ziara yake ya  kikazi ya kukagua uimarishaji mfumo wa huduma kwa wateja katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na Hospitali ya Sinza Palestina .

Dkt Gwajima amefafanua kuwa, mahala sahihi  kwa  kuripoti kero  za Wateja wakati wa kupata huduma ni kwa Mganga Mkuu wa Kituo, Mganga Mkuu wa Halmashauri, Mganga Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI na ikishindikana  Wizara ya Afya.

“ Ili kuhakikisha kero hizo zinafika kwa wakati  kila kituo cha kutolea huduma za afya (zahanati, kituo cha afya na hospitali ya Halmashauri) lazima kuimarisha mfumo mzima wa huduma kwa wateja kwa kutumia utaratibu wa kuweka namba za simu kwenye eneo la wazi linaloonekana hususani  wanapokaa wateja kusubiria huduma hivyo, wateja wahakikishe wanapata namba hizo na kuzitumia ili kusaidiwa kwa wakati”, amesisitiza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amesema kuwa wito huo  umekuja baada ya kubaini uwepo wa matukio ya baadhi ya watumiaji wa huduma za afya katika baadhi ya vituo kulalamikia kero walizokutana nazo wakati wa kupata huduma za afya huku muda mrefu ukiwa umepita hivyo, kukosa fursa ya kupata ufumbuzi kwa wakati.

Lakini pia Dkt Gwajima amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini ndani ya siku saba kuhakikisha mfumo huu unaimarishwa mara moja na taarifa zinawafikia wananchi wote wanaotumia huduma katika maeneo husika.

Kwa kuongezea Dkt. Gwajima amesema kuwa, kila zahanati, kituo cha afya na hospitali ya Halmashauri lazima iwe na bango kubwa lenye kuonesha namba maalumu ya simu ya kituo kwa ajili ya kushughulikia kero za wateja wanaokuja kupata huduma za afya vilevile, namba ya Mganga Mfawidhi wa Kituo husika, namba ya Mganga Mkuu wa Halmashauri, Mganga Mkuu wa Mkoa, namba za Ofisi ya Rais TAMISEMI na namba ya Kituo maalumu cha Simu (Call Centre) cha Wizara ya Afya ambayo ni 199.

“Na sisi kama Ofisi ya Rais TAMISEMI leo tunatangaza namba maalumu ya kupokea Kero na Pongezi kutoka kwa wateja juu ya utoaji huduma za afya katika hospitali zetu za ngazi ya afya ya msingi na namba hiyo ni 0734124191. Hivyo, iwapo Mteja utakuwa na Kero na hujapata msaada ngazi ya kituo, mganga mkuu wa halmashauri na mkoa basi usiondoke na kero yako bali haraka tuma ujumbe juu ya kero hiyo ukieleza uko Halmashauri gani na Kituo gani na sisi Ofisi ya Rais TAMISEMI tutakupigia na kuchukua hatua stahiki za kupata ufumbuzi juu ya kero hiyo kwa wakati sahihi” ameeleza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amebainisha kuwa lengo la kuimarisha huduma kwa Wateja ni kutatua kero zao kwa wakati na kuhakikisha kila mwananchi anayefika kwenye kituo cha huduma za afya ngazi ya msingi anafurahia huduma hizo na haondoki huku moyoni akiwa na manung’uniko yasiyo ya lazima.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amewapongeza wataalamu wa sekta ya afya nchini kwa kupokea kwa uzalendo na kutekeleza kwa vitendo mwelekeo wa kupambana na kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 kupitia maono makubwa ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa.

“Tuwe wabunifu na tupigane vita hii bila hofu na kwa kuzingatia mazingira mahsusi ya nchi yetu, Kupitia maono haya Covid 19 imedhibitiwa mapema sana na Tanzania imeandika historia duniani juu ya mbinu za ubunifu na uzalendo juu ya mapambano haya”ameeleza Dkt.Gwajima.

Dkt Gwajima amesema, jukumu liliko mbele ya wataalamu wa huduma za afya nchini  ni kuimarisha utekelezaji wa miongozo ya kinga kwa ujumla ili uzoefu uliopatikana uendelee kwa ajili ya kudhibiti magonjwa yote ya kuambukiza na kuipungizia Serikali mzigo wa kuhudumia wagonjwa ambao wangeepuka kuugua magonjwa hayo iwapo wangepata elimu ya kujikinga na kutekeleza kwa vitendo mfano kunawa mikono.

 “Tusiache kuendeleza hizi mbinu za usafi zinazolenga kujikinga na magonjwa ya kuambukiza hususan kunawa mikono ili tudhibiti na kutokomeza kabisa magonjwa hayo yakiwemo kipindupindu na magonjwa yote ya tumbo yatokanayo na kula vyakula kupitia mikono isiyo safi” amesisitiza Dkt. Gwajima.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Dkt.Rashid Mfaume amesema kuwa yeye kwa kushirikiana na watendaji wenzake ndani ya mkoa wa Dar es salaam ndani ya siku saba watakuwa wametekeleza agizo la kuhakikisha kunakuwa na mfumo na utaratibu wa kupokea na kushughulikia kero za wateja kwenye vituo vya huduma za afya kwa kutengeneza mabango makubwa yenye ubora wa kipekee yakionesha namba za simu zilizoelekezwa ili wananchi wafahamu na kuzitumia kwa wakati.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dkt. Delila Moshi akiahidi kutekeleza agizo hilo haraka sana kwa kusambaza mabango hayo kwenye maeneo yote muhimu waliko wateja huku akitumia mfumo wa matangazo ya sauti kuwafikia wateja wengi zaidi.

Kwa upande wake Mratibu wa Huduma za Dharura na Maafa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Christopher Mzava ametoa wito kwa wahudumu wa afya kuendelea kushirikiana kwa karibu na wateja ili kuweka mazingira mazuri ya kupokea mrejesho juu ya huduma wanazotoa kwa ajili ya kufanya maboresho




Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.