
WAKUU WA WILAYA WAASWA KUSIMAMIA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa, amewaomba wakuu wa wilaya nchini kusimamia kwa karibu zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa awali na msingi ili kuhakikisha mwanzoni mwa Januari 2026 wanaanza masomo kwa wakati.
Mhe. Kwagilwa ametoa maelekezo hayo leo, tarehe 28 Novemba 2025, mkoani Morogoro kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Msingi Juhudi iliyopo Mtaa wa Tushikamane katika Manispaa ya Morogoro.
Amesema usimamizi wa karibu kutoka kwa Wakuu wa Wilaya ni muhimu ili kuhakikisha watoto wote waliofikia umri wa kuanza shule wanandikishwa na hivyo kuondoa changamoto ya wanafunzi kubaki majumbani pindi masomo yanapoanza.
Aidha, Mhe. Kwagilwa amewataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo akisisitiza kuwa elimu ya awali ndiyo msingi wa mafanikio ya elimu ya mtoto katika ngazi zote zinazofuata.
Comments
Please sign in to leave a comment.

