
SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA KUWATAMBUA WADAU WA LISHE NCHINI
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Bw. Melkiori Baltazari, amesema ni muhimu kwa Serikali kujua wadau wa masuala ya lishe walipo na shughuli wanazotekeleza ili kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi katika maeneo yote ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Bw. Baltazari ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Maafisa Lishe wa Mikoa, kilicholenga kujumuisha taarifa za wadau wa lishe katika mfumo wa Wadau Portal, kilichofanyika mkoani Morogoro.
Amesema Serikali inapaswa kufahamu kwa usahihi wadau waliopo, miradi wanayoitekeleza, na maeneo wanayoyafikia ili kuepusha mkusanyiko wa wadau wengi sehemu moja huku maeneo mengine yenye uhitaji yakikosa huduma.
“Ni muhimu sana Serikali kujua wadau wetu wako wapi, wanafanya nini na maeneo wanayotekeleza miradi yao ili kuepuka wadau wengi kujazana sehemu moja na kushindwa kufikia maeneo mengine yenye uhitaji,” alisema Baltazari.
Aidha, Bw. Baltazari alieleza kuwa mfumo wa Wadau Portal umetengenezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa lengo la kusimamia na kukusanya taarifa za wadau wanaotekeleza miradi ya lishe katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hatua ya kuandaa mfumo huo imetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kupitia Idara ya TEHAMA na Kitengo cha Lishe, kwa uhisani wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme – WFP). Mfumo huo wa kidigitali unatarajiwa kuboresha uratibu, ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za lishe nchini.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
Tangazo la kuitwa kazini ajira za TMCHIP 2025
Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Takwimu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI - 2024/25 -2028/29
Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji 2024
Kanuni za Uchaguzi wa mwaka 2024
Tangazo la Uchaguzi

