
KAMATI YA UTAALAMU WA MIRADI YA UBIA WATAKIWA KULETA MATOKEO CHANYA
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uratibu wa shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Bw. Johnson Nyingi amehitimisha mafunzo ya utekelezaji wa miradi ya ubia kwa kamati ya wataalam ya miradi ya ubia na uchambuzi wa Miradi ya Kimkakati, (PPP Node) akieleza namna washiriki wanavyotazamiwa kuleta mabadiliko chanya baada ya mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tano Jijini Dodoma.
Katika maelezo yake ya kuhitimisha mafunzo hayo, Bw. Nyingi amesema mafunzo hayo yalijikita zaidi juu ya namna ya kuibua miradi ya ubia, uandaaji wa maandiko mbalimbali ya miradi na namna ya kuchambua miradi hiyo pamoja na utekelezaji wake.
Mafunzo hayo yamewashirikisha viongozi na wataalamu 30 wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI ambao wanaunda kamati ya wataalam ya miradi ya ubia na uchambuzi wa miradi ya kimkakati (PPP Node) kwa mujibu wa takwa la kisheria (Sheria ya ubia sura 103) linalotaka kuanzishwa kwa kamati hiyo.
Kwa mujibu wa Nyingi ambaye pia ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, mafunzo hayo yatafuatiwa na zoezi la kupitia na kuchambua maandiko mbalimbali ya miradi ya maendeleo yaliyopokelewa kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kipindi cha mwaka 2025.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
Tangazo la kuitwa kazini ajira za TMCHIP 2025
Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Takwimu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI - 2024/25 -2028/29
Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji 2024
Kanuni za Uchaguzi wa mwaka 2024
Tangazo la Uchaguzi

