Habari Michezo ya UMITASHUMTA inayoendelea kwa Mwaka 2015

30-Juni-2015.

Mpira wa miguu kwa wavulana ilikuwa Arusha na Mwanza ambapo Arusha walishinda mabao 4 -0, Tanga waliifunga Ruvuma 2-0, huku Morogoro ikiichabanga Tabora 1-0.Matokeo ya mpira wa wavu kwa wavulana yanaonyesha kuwa Tanga ilishinda Kigoma kwa seti 2-0, Dodoma ikaichapa Tabora seti 2-0, Rukwa ikaishinda Lindi seti 2-0, huku Njombe ikilazwa na Singida kwa seti 2-0, hali kadhalika Kilimanjaro ikichabangwa na Katavi seti 2-0

Kwa upande wa wasichana Lindi ikaifunga Iringa seti 2-0 , Morogoro ikashinda seti 2-0 dhidi ya Rukwa. Kwa upande wa mpira wa mikono kwa wavulana Mbeya ilichapa Simiyu mabao 13-7, Rukwa na Tanga zilifungana mabao 15-15 huku Dar es salaam ikaichapa Kagera mabao 27-3, Kilimanjaro ikaicharaza Singida mabao 12-10, na Dodoma ikaifunga Tabora mabao 17-11 na kwa wasichana Dar es salaam ikainyuka Rukwa mabao 7-6,Tabora ikaichapa Arusha mabao 7-5 na Morogoro ikashinda mabao 8-5 dhidi ya Mtwara, Simiyu ikaifunga Kigoma mabao 10-7, na Manyara imeicharaza Iringa mabao 9-1.

Kwa upande wa mpira wa Netiboli Morogoro imeifunga Kilimanjaro mabao 43-13, Mtwara ilifungwa mabao 22-23 dhidi ya Katavi, Geita iliichakaza Pwani mabao 38-19 na Iringa ilicharazwa na Mbeya mabao 12-33m hali kadhalika Singida ilichabangwa na Mara mabao 12-33Mwisho,

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.