Jafo Azindua Kampeni ya “Sema Usikike” Apiga Vita Mimba za Utotoni.

Na.Fred Kibano

Jafo azindua kampeni sema usikike dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Selemani Jafo amezindua kampeni ya Kitaifa ijulikanayo kama Sema Usikike mjini Dodoma ambapo amewataka Wadau mbalimbali wajitokeze kuunga mkono kampeni hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Creative Plan (CP) inayotoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa.

Waziri Jafo amesema ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Taasisi hiyo na nyinginezo katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa, lakini pia amewataka walimu kusimamia kampeni hii kwa pamoja na kuwapa watoto uhuru na fursa kuzungumza mambo yanayo wakwaza katika upatikanaji wa elimu ikiwemo rushwa.

Waziri Jafo alisema kupitia Taasisi ya TAKUKURU nchini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli, Tanzania imetangazwa kuwa nchi ya 103 kutoka 117 katika suala zima la kupambana na rushwa. “rushwa imekua tatizo kubwa katika sekta mbalimbali, bila kupambana nayo watoto hawataweza kupata elimu iliyo bora”

Wakati huo huo Waziri Jafo amezindua kampeni ya kuzuia mimba za utotoni inayoendeshwa na wizara ya Afya, Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto ambapo aliipongeza wizara hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya kwani watoto wasipolindwa hapatakua na Viongozi wazuri hapo baadaye, lakini pia amewataka wananchi kushiriki kwa pamoja utekelezaji wa kampeni hizi mbili.

Kuhusu kuende;leza utamaduni wa Mtanzania Mhe. Jafo aliwaagiza Maafisa Utamaduni wote nchini waakikishe wanaweka utamaduni wa kutengeneza nyimbo zenye mahudhui ya kupambana na rushwa ili kujenga picha nzuri katika vichwa vya watoto siku zote jambo ambalo litajenga Taifa lisilo na rushwa nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Creative Plan, Juma Mtetwa alisema, “Dhumuni kubwa la kampeni hiyo ni kutolewa mashuleni ili kutoa elimu dhidi ya kupambana na rushwa” kwani kwa kufanya hivyo tutapata Taifa lenye weledi wa kupambana na suala zima la rushwa.

Suala zima la mimba za utotoni limekuwa changamoto ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya malezi ya watoto.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.