Mhe. Jafo akataa Kuzindua Mradi uliohujumiwa na Wananchi Utakaowahudumia

Na Fred Kibano

Jafo akataa Kuzindua Mradi uliohujumiwa na Wananchi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani S. Jafo, amekataa kuzindua Mradi wa maji wa kijiji cha Itiso kilichopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma baada ya kuonekana kuhujumiwa kwa Mradi huo wa mamilioni ya shilingi na wananchi wenyewe.

Mheshimiwa Jafo amekataa kuzindua mradi huo ambao umekuwa ukihujumiwa na wananchi wachache wasio waaminifu na badala yake ameutaka Uongozi wa wilaya ya Chamwino kuhakikisha wanachukua hatua kwa wale wote watakaobainika kuhujumu miundombinu ya mradi wa maji kijijini Chamwino.

“mimi sio mtu wa kupelekwa na mabango wakati wakati nyie wenyewe mnaharibu miundombinu ya maji. Hivi ni nani anayekata valvu na mabomba kama si nyie watu wa Itiso? Mnakata kwa makusudi ili kukwamisha mradi ambao Serikali imewekeza fedha nyingi. Hamjui kuwa kuna watanzania wengine wanahitaji mradi kama huu? Alisisitiza Waziri Jafo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Chilomwa Mhe. Joel Mwaka amesema changamoto kubwa ya mradi huo ni maungio ya mabomba na valvu ambayo yanavujisha maji suala ambalo wataalam wanalishughulikia lakini pia jamii ya hapa inapaswa kulinda miundombinu hii inayojengwa na Serikali.

Akisoma taarifa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, Mhandisi wa Maji Godfrey Mbabaye amesema Halmashauri Mradi wa maji katika kijiji cha Itiso ulianza kujengwa mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2014, mradi ambao ulijengwa na kampuni ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam mshauri Q & A Company Ltd. Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi milioni 338,676,323 ukihusisha kazi za ujenzi wa nyumba ya mashine, tenki la kuhifadhia maji ujazo wa lita 80,000, ulazaji wa bomba kilomita 15.9, ujenzi wa uvunaji maji ya mvua katika zahanati na msikiti, vichoteo 10 vya maji na ufungaji wa mitambo ya kusukumia maji.

Pia Mhandisi Mbabaye alisema Kazi zote zilikamilika lakini kulikuwa na changamoto za kuvujisha maji sehemu za maungio kwenye bomba la kuzambazia maji kutoka kwenye tanki.

Amesema Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya chamwino imefanya marekebisho kadhaa ili kuuboresha mradi huo kuwa na tija. “ Iliendelea kufanya marekebisho ya kutoa viungio vya mabomba vinavyovuja na kuchoma bomba kwa kutumia fusing machine kazi ambayo imekamilika kwa aslimia 95 na vichoteo 8 vinatoa maji”

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Itiso, Petro Mukune, amesema uharibifu huo wa miundombinu ya maji unafanywa na wananchi lakini litawekwa sanduku la maoni ili wananchi wapige kura na kuwapata wahusika.

Mradi huo wa maji ulitarajiwa kuwanufaisha wakazi wapatao 5,817 kupata huduma ya maji safi na salama ambao wamekuwa wakichota maji katika visima vya kienyeji na makorongo.

Katika ziara yake ya mwezi Agosti, 2017 Waziri wa Nchi Ofisi Rais TAMISEMI, Selemani S. Jafo aliagiza changamoto hiyo itatuliwe na Mkandarasi akishirikiana na Mtaalamu mshauri pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Chamwino baada ya kumtoa Mkandarasi ambaye alishindwa kujenga kwa kiwango kinachotakiwa.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.