Jafo awataka Wadau wa Elimu kuunga mkono Sera ya Elimu Bila Malipo

Na.Fred Kibano

Serikali yahimiza wadau kuunga mkono elimu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo amewataka Wadau wote wa Elimu pamoja na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali kutekeleza sera ya elimu Bila Malipo.

Mhe. ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya shule katika shule ya msingi Uguzi, iliyopo wilayani Chamwino, mkoani Dodoma. Vifaa hivyo vilitolewa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Dkt. Ombeni Msuya na Abdallah Jacob kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Amewataka wadau hao wasikate tamaa kuunga mkono Serikali kuhusu Elimu, alisema “japo changamoto ni nyingi lakini wanafunzi wenye uhitaji maalum wanahitaji msaada wao”. alisisitiza wanafunzi wengi wanakosa fursa ya vitendea kazi kama madaftari na kalamu hivyo ni jambo la msingi kwa wadau wa elimu kuendelea kusaidia watoto hao na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza sera ya Elimu Bila Malipo.

Waziri Jafo pia alizindua mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu” amesema ujumbe huu unamuhusu mtoto mwenye uhitaji wa kupata elimu ameomba Watanzania kwa ujumla kuunga mkono jambo hili.

Aliwaomba wadau hao wasichoke na wasikate tamaa kuchangia kwani watoto wengi wamepotea kwa kukosa vitedea kazi hivyo ni vyema kuwaokoa watoto hao na kuwatoa kwenye mazingira hatarishi. Hivyo ni vyema watanzania kuwaunga mkono wadau wa elimu kwani wameongeza knguvu kazi kwa serikali kuwapatia elimu watoto wenye uhitaji.

Japo kuna changamoto kubwa lakini ni vyema kujikita zaidi kusaidia Umma na kuunga mkono kutatua changamoto za elimu. Alisema wengine ni yatima hawapati mahitaji maalum ya shule hivyo wakisaidiwa itakua ni jambo la muhimu sana. Amewashawishi Watanzania kushirikiana kwa pamoja kusaidia mpango huu ambao utawasaidia watoto wenye mahitaji maalum.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.