NZUNDA AWAASA WASIMAMIZI NA WATENDAJI WA ELIMU UPOTOSHWAJI WA KAULI YA MHE. RAIS MICHANGO MASHULENI

Serikali yataka kutoitafsiri kauli ya Mhe Rais vibaya
--------------------------------------------------

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tixon Nzunda ameyafunga mafunzo ya Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (Education Programme for Results – EP4R) kwa watendaji na wasimamizi wa Elimu mjini Dodoma.

Akifunga mafunzo hayo ya wasimamizi wa elimu kwa ngazi ya Mikoa, Kanda na Halmashauri Nzunda amesema tangu utekelezaji wa programu ilipoanza mwaka 2014, Halmashauri zimepokea jumla ya shilingi bilioni 77.98 zilizotolewa kamamotisha wa utekelezaji wa EP4Rkutoka kwa wafadhili ambazo zimetuka katika kuboresha utoaji wa elimu katika shule za Serikali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na samani za shule, kurekebisha ikama ya walimu, utoaji wa motisha kwa walimu na kuwezesha ufuatiliaji.

“tangu kuanza kwa Programu hii mwaka 2014 Mamlaka za Serikali za Mitaa zilipokea shilingi bilioni 77.98 ambapo kwa mwaka 2014/2015 shilingi bilioni 15.53, mwaka wa pili 2015/2016 shilingi bilioni 22.36 na mwaka wa tatu 2016/2017 shilingi bilioni 40.09 zimetolewa kama motisha wa utekelezaji wa EP4R toka kwa wafadhili”

Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu Nzunda amewataka watendaji hao kutoa ufafanuzi kwa wananchi na watu mbalimbali kuhusu michango ya shule kwa kuwa kauli hiyo inapotoshwa na kuleta mkanganyiko kwa jamii. “kama wananchi wana nia ya kuchangia michango kwa hiari yao kwa lengo la kuboresha lishe shuleni, basi wachangia kwa ridhaa yao wenyeewe, wawe na kamati yao nje ya mfumo wa shule” Hivi karibuni, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipiga marufuku michango mashuleni kwa lengo la kumwondolea mzazi mzigo wa kulipia gharama za kielimu ambazo Serikali imebeba dhamana hiyo.

Aidha, amewataka Maafisa Elimu na Wakurugenzi kuwasaidia wathibiti ubora (wakaguzi wa shule) ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa wakati ili kuinua kiwango cha elimu nchini kama sekta hiyo muhimu ilivyo ainishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Utekelezaji maagizo ya Viongozi kwa wakati kama vile masuala ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwamba fedha zisikae katika akaunti “nisingependa fedha hizo zikae ktk acc ninapenda fedha hizo zikaanze kutumika ili wanafunzi wakaanze kukaa katika majengo na ndani ya kipindi cha miezi mitatu majengo hayo yawe yamekamilika, tunakwenda kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Hatutakuwa na msamaha kwa Mkurugenzi ambaye fedha zimekaa kwenye akaunti na wanafunzi hawana miundombinu ya kutumia mashuleni” amewataka pia kuwatumia Maafisa Habari wa Halmashauri kutangaza masuala mbalimbali ya Halmashauri kama sehemu ya mafanikio ya Serikali.

Nzunda amewataka watendaji na wasimamizi wa elimu kuendelea na utekelezaji wa programu ya EP4R kwa ufanisi ili kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano kwa, “kufuata miongozo na maelekezo ya matumizi ya fedha ili kuepuka hoja, ujenzi wa majengo ya shule uzingatie ramani zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Halmashauri zote kuhakikisha zinasambaza walimu ili kuwa na uwiano unaokaribia kwa shule zote, Halmashauri zifanye uchambuzi kuona halmashauri zenye vitabu vingi na ambazo hazina vitabu ili kuvisambaza vilivyozidi kutoka kwenye shule zenye ziada na kwenda shule zenye upungufu, Halmashauri zihakikishe shule zinakaguliwa kwa wakati muafaka”

Akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi, Mratibu wa Programu ya EP4R ofsisi ya Rais TAMISEMI, Newaho Mkisi amesema kuwa mafunzo hayo yamefanyika nchi nzima na yalianza tarehe 15 Januari, 2018 katika vituo vya Dar es Salaam, Mbeya na Arusha ambapo kituo cha Dodoma kilichohusisha mikoa ya Moroforo na Dodoma ndicho kituo cha mwisho kupatiwa mafunzo. Amesema jumla ya washiriki 775 wamepatiwa mafunzo nchi nzima wakiwemo Wathibiti ubora wa shule wa kanda na wilaya, pamoja na Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari.

Katika mafunzo haya elekezi washiriki wamewezeshwa mada mbalimbali kuhusu Programu ya Lipa kulingana na Matokeo na utekelezaji wakepamoja na vigezo vya upimaji na utoaji motisha katika ngazi za Kitaifa na Halmashauri.

Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo inatekelezwa kwa pamoja kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo tangu kuanza kwake miundombinu mbalimbali ya majengo imejengwa, ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na fedha za motisha lengo likiwa ni kuboresha sekta hiyo muhimu nchini.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.