Jafo apongeza Jitihada za Mbunge wa Makambako

Na. Nteghenjwa Hosseah

Serikali yapongeza ujenzi wa ofisi za madaktari Njombe Mji

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako, Mhe. Deo Sanga kwa jitihada mbalimbali anazozifanya katika kuboresha Sekta ya Afya katika Jimbo hilo. Jafo ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospitali ya Mji wa Makambako na kuona vyumba viwili vya Madaktari ambavyo vimejengwa na Mbunge huyo, Mhe. Sanga. "Kwa dhati kabisa nimpongeze Mhe. Sanga, kwa kujitoa kuboresha huduma za Jamii hii inaonyesha nia yake njema katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa sababu wananchi wakiwa na Afya Njema wataweza kuendelea na shughuli zao kikamilifu za kujitafutia kipato kasha kupata maendeleo" Alisema Jafo

Kwa kutambua idadi kubwa ya watu wanaopata huduma katika Hospitali hiyo ambayo ina miundombinu duni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa jengo la kisasa la Kuhifadhia maiti pamoja na ukosefu wa wodi mbalimbali. Waziri Jafo amesema Serikali itaangalia jinsi ya kuboresha miundombinu hiyo ili wakazi wa Makambako waweze kupata huduma bora za Afya kama wanazopata Watanzania wengine. "Tutaweka Jitihada katika kutafuta fedha kutoka kwenye vyanzo vyetu ili kuongeza miundombinu ya Afya na hospitali hii iweze kuwa na hadhi ya kuwa na Hospitali ya Mji" Alisema Jafo.

Hata hivyo Jafo amechukua kilio cha Hospitali hiyo kuendelea kupata mgao wa Kituo cha Afya wakati imeshapandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Mji na ameahidi kulishughulikia. "Makambako ni eneo muhimu sana katika Kanda hii yenye wakazi wengi, shughuli nyingi za kiuchumi na muingiliano wa watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo inahitaji huduma bora Zaidi za Afya kwa kuzingatia umuhimu wa eneo na wananchi wake" alisema Jafo.

Waziri Jafo anaendelea na ziara yake katika Mikoa Mbalimbali lengo likiwa ni ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ipo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, zinazosimamiwa na Mikoa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ujumla.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.