Waziri Jafo Akemea Utatu Usio Mtakatifu katika manunuzi ya kazi za TARURA

Na Nteghenjwa Hosseah

Serikali yawataka watendaji TARURA kufanya kazi kwa weledi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watumishi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuvunja utatu usio mtakatifu katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara zinazoendelea kutangazwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kufungua mafunzo ya siku sita ya watalaam wa TARURA kutoka katika Mikoa saba ya Nyanda za Juu kusini kuhusiana na masuala ya ununuzi wa Umma na usimamizi wa Mikataba ya Ujenzi na matengenezo ya barabara na Maadili katika kazi za TARURA yenye takribani miezi sita sasa tangu kuanzishwa kwake.

Waziri Jafo anasema, "Ninaposema Utatu usio mtakatifu namaanisha Afisa Manunuzi,Mhasibu na Mhandisi wa TARURA katika eneo husika hawa ndio huwa wanaamua nani apewe kandarasi kwa mujibu wa mahusiano na makubaliano wanayoyajua wao. "Huu Utatu usio mtakatifu katika kazi za Umma ufe kuanzia leo na Mkandarasi apewe kazi kwa kuzingatia uwezo wake wa kitaalam na kifedha katika kukamilisha kazi hiyo na sio mahusiano na makubaliano nje ya vigezo vilivyowekwa"

Katika Utatu huu ninauouzungumzia kuna mahusiano ya karibu sana na rushwa na inafahamika wazi kuwa rushwa hupofusha wataaalam kuona na kutathmini uwezo wa Mzabuni, huzorotesha kazi iliyopangwa kufanyika na kuwanyima wananchi haki yao ya Msingi ya huduma bora za barabara na tutakao wabaini wakiendeleza kasumba hii tutawachukulia hatua za kisheria na kinidhamu, alisema Jafo.

Akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala amesema wamejiandaa kikamilifu kusimamia kazi za TARURA na baada ya uzinduzi wa kitaifa walizindua tena Kimkoa ili kuwafahamisha wananchi wa Mkoa huu umuhimu wa Taasisi hii, ili waweze kumiliki Kazi zinazofanywa na TARURA na kuwaelewesha lengo la kutaka kazi za barabara kutoka Halmashauri na kusimamiwa na TARURA.“TARURA imekuja kuboresha kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na Baraza la Madiwani, Kamati za kudumu pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi sasa TARURA wamekuja kutekeleza kitaalam zaidi, namna ya usimamizi, manunuzi, mikataba ili tuweze kupata matokea bora na ya haraka.

Naye Mkurugenzi wa TARURA Mhandisi Abdul R. Digaga amesema mafunzo haya ni mpango wa Kimkakati wa TARURA katika kupambana na rushwa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya barabara, mgongano wa maslahi, matumizi mabaya ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara na ukosefu wa Uadilifu miongoni mwa watendaji.

Mafunzo hayo ambayo yalianza kufanyika katika kanda mbalimbali nchini na kanda hii ya Nyanda za juu kusini ni ya mwisho kufanyika kwa wataalam wa TARURA wa kada mbalimbali na imejumuisha Mikoa ya Mbeya, Songwe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Iringa na Njombe.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.