Washirikisheni Wananchi katika Miradi ya Maendeleo

Na Fred J.Kibano

Mhe Kakunda ataka ushirikishwaji wananchi katika miradi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Kakunda amewataka Viongozi wa Sekta ya Elimu kutumia nguvu za wananchi ‘force account’ na mafundi wadogo wadogo wazawa katika miradi midogo ambayo wakipewa Wakandarasi wakubwa hutumia fedha nyingi.

Mhe. Kakunda ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro katika wilaya za Siha na Hai ili kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa hususani Miradi ya maendeleo ya sekta ya Elimu na maji.

“katika elimu tatizo kubwa ni miundombinu, wananchi waendelee kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zilizopo, matumizi ya force account na mafundi wa kawaida wakitumiwa vizuru wana tija katika kujenga madarasa, vituo vya afya, ofisi na miundombinu mingine bali wakandarasi wabakie na majengo makubwa”

Aidha, amekemea kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kupewa ujauzito kuwa ni jambo la aibu na halikubaliki kwani changamoto ya suala hili ni sheria ambayo imekuwa ikifanyiwa marekebisho toka katika sheria ya mwaka 1978. Amesema kwa kuwa wahusika wakipata dhamana kazi wanayoifanya ni kuharibu ushahidi na hivyo kufanya eneo la ushahidi kusumbua katika suala zima la sheria na hivyo wazazi ndio wahusika wakuu lakini kwa kuwaelimisha wazazi tatizo la mimba mashuleni litapungua. “Waambieni wazazi katika mikutano ya shule waache kuwaachia wabakaji”

Akiwa katika sekondari ya Harambee iliyopo wilayani Hai, Mhe. Kakunda amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na maarifa na kufikia malengo waliyojiwekea pasipo kukatisha masomo. Wilayani Siha Mhe. Kakunda ameshangazwa na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kwa shule za msingi baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya wilaya hiyo na Mkuu wa wilaya ya Siha, kwa madai ya kuwepo kwa idadi kubwa ya feki iliyopunguza ikama ya walimu na kufanya ufaulu ushuke hadi kufikia asilimia 69.5, sababu nyingine zilizotajwa ni pamoja na jamii kuhamahama mara kwa mara na hali ya ufundishaji wa wanafunzi isiyo ridhisha.

Kuhusu mapato ya Halmashauri ya Siha, Mhe. Kakunda amewataka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya kufanya bidii ya kukusanya mapato ili wafikie asilimia 80 au zaidi kwani hamashauri inapimwa kwa ukusanyaji wa mapato.

Katika hatua nyingine Mhe. Kakunda ameagiza kurudiwa kwa mchakato wa maamuzi ya Baraza la Madiwani urudiwe kwa kuwa uliingia dosari kwa kuwarejesha kazini Maafisa wa Halmashauri ya Siha kazini ambao walihujumu mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo. “naagiza mchakato wa upigaji kura uliofanywa na Baraza la Madiwani urudiwe, ili kama wahalifu watatetewa nao tujue. Ni aibu kwa Baraza la Madiwani kutetea wahalifu, hili ni tatizo, Halmashauri inaishi kwa mapato bila mapato mnaua halmashauri, angalau basi muwe kati ya asilimia 50 hadi 80, hii ni hatari”

p align="justify"> Akiwa wilayani Siha Mhe. Kakunda amefungua bweni moja la sekondari ya Nuru lenye uwezo wa kupokea wananfunzi 48 na kuwasihi wanafunzi kuitunza miundombinu hiyo kwani Serikali hutumia fedha nyingi, pia amekagua majengo ya vyumba viwili vya maabara vilivyopo katika hatua ya mwisho na kuagiza vikamilke na kuanza kutumika kwa wakati ili wanafunzi waweze kujifunza kwa vitendo.

p align="justify"> Pia amekagua ujenzi wa madarasa mawili na msingi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo manne katika shule ya sekondari Esinyai, lakini shule hiyo haijafunguliwa kutokana na sheria ya elimu inayotaka walau madarasa mann, ofisi na matundu ya vyoo kuwa yamekamilika ambapo amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa kufuatilia suala la usajili wa muda ili wanafunze waanze masomo yao.

p align="justify"> Mhe. Kakunda amemaliza ziara yake Mkoni Kilimanjaro na kuanza ziara mkoni Arusha ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.