MHE. KAKUNDA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI KUNUFAISHA WANANCHI

Mhe Kakunda ahimiza Viongozi kusimamia Miradi ya vya maji
--------------------------------------------------

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Kakunda (Mb) ameendelea na ziara yake mkoa wa Kilimanjaro na kujionea utekelezaji wa baadhi ya Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri za Same, Mwanga, Hai na Siha. Akiwa wilayani Mwanga Mhe. Kakunda amekagua Mradi mkubwa Kitaifa wa maji safi wa Same – Mwanga – Korogwe unaotekelezwa na Serikali na Wafadhili ili kuondoa kabisa tatizo la maji katika wilaya za Same, Mwanga na baadhi ya vijiji vya wilaya ya Korogwe, hii ikiwa ni pamoja na vijiji 38 vinavyozunguka eneo la mradi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Kakunda amewataka Viongozi wa Wizara, Mkoa na Wilaya kusimamia Mradi wa maji kwa karibu kwa kuwa Serikali inataka kuona thamani ya fedha katika miradi na pia inatumia fedha nyingi katika mradi huu. “Serikali inatumia fedha nyingi katika mradi huu na miradi mingine ya maji, hivyo Wahandisi na Viongozi wote hakikisheni mnafuatilia kila mara hatua zote za mradi huu, ili mradi ulete tija kwa wananchi”

Mradi huu Mkubwa unatarajiwa kunufaisha jumla ya wananchi 438,931 ambao 246,793 wapo Same, 177,085 wapo Mwanga na 15,053 wapo wilaya ya Korogwe. Gharama za Mradi zinakadiriwa kuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 42.3 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 900.

Utekelezaji wa mradi katika hatua ya kwanza umefikia asilimia 65.49 na Mkandarasi anatakiwa kukamilisha Mradi huu mwezi Mei, 2018. Mradi huu ukikamilika utakuwa na uwezo wa kutoa lita za maji zipatazo milioni 103.68 kwa siku wakati mahitaji ya wakati huu ni lita milioni 78.38

Mheshimiwa Kakunda amepongeza kazi zinazoendelea za ujenzi wa chanzo cha maji kando yam to Pangani chini ya Bwawa la Nyumba ya Mungu, uchimbaji wa eneo la matenki ya kuhifadhia maji lita zipatazo milioni 9 katika mlima Kivengere, vituo ambapo pampu zitajengwa, utandazaji wa mabomba katika awamu ya kwanza na Changamoto za Mradi ni pamoja na kuchelewa kwa malipo kutoka kwa Wafadhili na kusababisha ongezeko ya gharama ya riba inayotozwa na Wakandarasi kwa kucheleweshewa malipo yao na pia kuongezeka kwa gharama ya muda wa usimamizi kutokana na nyongeza ya muda wa mkataba wa Mkandarasi aliopewa kufidia kupotea kwa kucheleweshewa malipo.

Katika hatua nyingine Mhe. Kakunda amekagua Mradi wa maji ya Kisima kilichochimbwa kwa ufadhili wa Serikali ya Misri ambapo kwa mwaka 2016/17 Serikali ilitoa shilingi 80,400,000 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji wilayani Same, hali inayopelekea kuongezeka kwa huduma ya upatikanaji wa maji wialyani Same.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.