SERIKALI YASITISHA MKATABA WA MAKANDARASI MAGINGA BUSINESS HOLDING Co. L.t.d ,TARURA YAPEWA JUKUMU LA KUFUATATILIA.

Na. Angela Msimbira

SERIKALI YASITISHA MKATABA WA MAKANDARASI TARURA YAPEWA JUKUMU LA KUFUATATILIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Seleman Jafo amesitisha mkataba wa Mkandarasi Maginga Business Holding Co. L.t.d aliyekuwa akijenga barabara kutoka Namelock hadi Lopeltes kwa kushindwa kumaliza ujenzi huo kwa wakati wilayani Kiteto , Mkoani Manyara

Akikagua barabara hiyo Mhe Suleman Jafo amesema hajarizishwa na kazi inayofanywa na Mkandarasi Maginga Business Holding Co. Ltd ambaye anajenga barabara ya kutoka Namelock hadi Lukelo kwa kuwa mkataba wake ulianza tangu tarehe 17/6/2017 na kupewa miezi Tisa kukamilisha kazi hiyo lakini mpaka leo barabara yenye kilometa 44.1 imesafishwa kilometa kumi na saba, hivyo dhamani ya kazi iliyotekelezwa hadi sasa ni asilimia saba

Amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA Bw. Victor Seif kuhakikisha wanaongea ndani ya siku saba ili kupata muafaka wa ujenzi wa barabara hiyo na asipojitokeza atolewe kwenye lisiti ya wakandarasi ambao hawataruhusiwa kufanyakazi za TARURA nchi nzima.

Amesema kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imepewa dhamana ya kusimamia na kutekeleza ujenzi wa miundombinu kwa kuona hivyo imeanzisha wakala maalum wa kusimamia ujenzi wa barabra vijijini (Tarura) lengo likiwa ni kusimamia ujenzi wa barabara katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, barabara za vjijini na mijini

“Hakutakuwa na masiahara yeyote fedha zinazotengwa hizi zitasimamiwa kwa kiwango kisichorizisha, Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyakazi wazembe ambao hawataki kuwafikia wananchi ili wapate huduma nzuri

Amesema barabara hiyo ya Namelock hadi Sunya itajengwa kwa kiwango kinachotakikana na Serikali na lengo la serikali ni kujenga barabara ili uchumi wa kiteto uweze kupanda kutokana na miundombinu ya barabara iliyowekwa na Serikali

Amesema kuwa Maginga construction alipewa siku ishirini na nane kwa ajili parfomance appraisal lakini hakufanya hivyo hii inaonyesha kuwa si mwaminifu na uwezo wake wa kufanya kazi hauendani na kiwango cha kazi kilichotekelezwa, hivyo fedha ya serikali ingepotea na barabara ingekuwa haipo katika ubora unaotakiwa

Amesema barabara hiyo inatumia zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka Namelock hadi Sunya,ukilinganisha na barabara zote zilizotengenezwa yenyyewe inatumia fedha nyingi hivyo mkandarasi ameonyesha dhahiri kwamba hakuweza kutekeleza kazi alizopewa katika mkataba wake na Serikali

Ameiagiza TARURA kuwaangaliwa wakandarasi ambao si waaminifu kutokupewa tenda za ujenzi wa barabara nchini kwa kuona kuwa serikali ndio kichaka cha wadanganyifu kwa kuwa hivi sasa Serikali haitaji makanjanja katika suala zima la ujenzi wa barabara nchini.

Amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Taruara kuhakikisha mkandarasi huyo hapati kazi yeyote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,na kuwaonya wakandarasi wengine kutokufanyakazi kwa ubabaishaji bali wafanye kazi kwa weledi ili kutimiza malengo ya serikali ya ujenzi wa miundombinu bora kwa jamii.

Aidha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia miradi ya maendeleo nchini ili dhamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na dhamani ya miradi inayotekelezwa nchini.

Mhe. Jafo amesema kazi kuu ya Wakuu wa Mikoa nchini ni kusimamia maagizo yanayotolewa na serikali hasa katika suala zima la kusimamia maendeleo katika maeneo yao ili fedha zinazotolewa ziendane na kazi zinazotekelezwa katika jamii

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Bw. Victor Seif amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua wakandarasi ambao wanaenda kinyumbe na mikataba wanayopatiwa na Serikali hasa katika suala zima la ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha iliingia makubaliano na shirika la kimataifa la Maendeleo la Marekani USAID kufadhili miradi ya barabara katika wilaya za Mvomero, Kilombero, Kongwa na Kiteto kwa mwaka wa fedha 2014/2018.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.