Waziri Jafo aipongeza Manispaa ya Temeke

Na Nteghenjwa Hosseah

Waziri Jafo aipongeza Manispaa ya Temeke

Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amepongeza uongozi wa Manispaa ya Temeke kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na maagizo mbalimbali ya Serikali.

Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Jengo la Utawala na Maabara itakalotumiwa na wataalam wa mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(DMDP) kutekeleza shughuli mbalimbali za mradi mpaka hapo utakapokamilika.

Amesema Mradi huu unatekelezwa katika Manispaa zote za Jiji la Dar es salaam lakini Manispaa ya Temeke mmekuwa wa kwanza kukamilisha Jengo hili na leo nalifungua rasmi ili lianze kutumika kwa kazi mbalimbali za mradi.

“Temeke sio tu mmetekrlrxa kwa ufanisi mradi huu lakini hata maagizo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa Serikali na mimi mwenyewe ni shahidi kwa sababu nilishapita zaidi ya mara tatu na kuagiza kazi mbalimbalina ninaporudi baada ya siku kadhaa nakuta mmetekeleza kwa kiwango kinachostahili” alisema Jaffo.

Waziri Jafo aliwataka viongozi wa Manispaa zingine kuja kujifunza kutoka Manispaa ya Temeke namna ambavyo wamekuwa makini kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mradiwa Uendeezaji wa Jiji la Dar es Salaam unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na utahusisha Ujenzi wa barabara kilometa 210 kwa kiwango cha lami kwenye maeneo mbalimbali yanayounganishwa na ukanda wa mabasi yaendayo haraka, maeneo yanayounganisha Wilaya na mkoa kwa ujumla pamoja na maeneo yaliyojengwa kiholela kwenye kata 14 zilizoainishwa.

Mradi huo pia utajenga kilometa 40 za mifereji mikubwa ya kutiririsha maji ya mvua ili kudhibiti changamoto za mafuriko ujenzi wa ofisi 3 za kudumu zenye gorofa 1 katika Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni pamoja na maabara za kisasa za kupima viwango vya ujenzi pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kutunza mifumo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato na mifumo ya upimaji na utunzaji wa taarifa za kijiografia (GIS)

Zaidi ya hapo DMDP itapandisha hadhi maeneo yaliyojengwa kiholela katika kata 14 za Tandale, Mburahati, Mwananyamala, Gongo la Mboto, Kiwalani, Ukonga, Keko, Kilakala, Mbagala kuu, Mbagala, Mtoni, Yombo vituka, Kijichi na Makangarawe. Huduma zitakazopelekwa katika kata hizo ni kuweka taa za barabarani, ujenzi wa mifereji ya kutitirisha maji, ujenzi wa njia za watembea kwa miguu, kuweka nyenzo za ukusanyaji taka ngumu kwa kununua magari ya kusomba taka na ununuzi wa vizimba vya taka, ujenzi wa masoko, ujenzi wa vituo vya mabasi. kujenga maeneo ya mapumziko, huduma za vyoo vya umma na huduma za maji safi na upimaji wa viwanja zaidi 800 vyenye miundombinu ya kijamii katika eneo la Vikunai kata ya Tuangoma Manispaa ya Temeke.

Halkadhalika Mradi utasaidia kuimarisha uwezo wa kitaasisi wa Manispaa za jiji la Dar es salaam kwa kuboresha Mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuainisha na kuibua miradi jumuishi ya njia za usafirishaji jijini na matumizi bora ya ardhi kwa kuibua aina mbalimbali za vivutio vya uwekezaji katika ukanda wa mabasi yaendayo haraka, kuimarisha mifumo ya ujenzi na matengenezo pamoja na kuimarisha mifumo ya mipango miji katika ngazi zote kwenye Manispaa za jiji; Kuandaa na kutekeleza Mpango Kabambe wa mfumo wa maji taka na maji ya mvua katika mkoa wa Dar es salaam (Dar es salaam Drainage and Sewerage Master Plan 2016 -2036).

Aidha, mradi utasaidia kujenga uwezo kwa manispaa katika usimamizi wa miradi mikubwa hasa kwenye nyanja za manunuzi, usimamizi wa fedha, masuala ya mazingira, ukaguzi, ufuatiliaji na tathmini.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.