Halmashauri ya Mbeya yatakiwa kuwachukulia hatua mkandarasi na watumishi wazembe

Na Angela Msimbira

Halmashauri yatakiwa kuchukua hatua kwa uzembe wa watumishi Serikali

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Joseph Kakunda ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya mbeya kuwachukulia hatua za kisheria watumishi na kumfungia Mkandarasi aliyejenga daraja la Idiwili lililopo Mkoani kutokufanya kazi katika halmashauri yeyote nchini Tanzania.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kubaini changamoto za utendaji kazi katika miradi ya maendeleo na kubaini chanzo cha migogoro ya kiutawala iliyopo katika halmashauri ya Mbeya na Tundu inayofanyika Mkoani Mbeya Mhe. Joseph Kakunda amesema uzembe uliofanyika ni wa kiwango cha juu na kuisababishia hasara Serikali

Amesema kuwa daraja la Idiwili limejengwa chini ya viwango kiasi kwamba limeanza kukatika kabla ya kuanza kutumika kitendo ambacho ni uzembe uliosababishwa na watumishi wa Halmashauri hiyo pamoja na Mkandarasi. “Ninaagiza watumishi wote waliohusika na ujenzi wa mradi wa daraja la Idiwili kuchukuliwa hatua kulingana na taratibu za kiutumishi, pamoja na mkandarasi aliye husika na ujenzi huo kusimamishwa kufanya kazi katika halmashauri zote nchini.” Amesema Mhe. Kakunda.

Katika zira hiyo Mhe. Kakunda aliongea na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kuwaagiza kufanya kazi kwa weledi wakifuata sheria, kanuni na taratibu ili kupata matokeo hasi katika kutoa huduma kwa jamii. Akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mhe Joseph Kaganda amesema watumishi wote anawajibu wa kufuata sheria na taratibu katika kutoa huduma kwa jamii ili kuwawezesha kutoa huduma stahiki kwa jamii wanayoihudumia. Watumishi watumie weledi katika kutekeleza maagizo yanayotolewa na serikali.

Akiongea na wananchi wa Tunduma waliomsimamisha kutaka kutatuliwa kero ya kiutawala Mhe. Joseph Kakunda amesema serikali imelichukua suala hilo na kulifanyia kazi kwa haraka ili kuleta Amani katika Wilaya ya Tunduma Mkoani Songwe. Akiongelea kuhusu sula la maji amezitaka halmashauri kuhakikisha wanasimamia kwa karibu umaliziaji wa miradi 8 inayoendelea ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa na kuwachukulia hatua wote waliosababisha miradi ya maji kuchelewa kukamilika.bani Akiwa njiani kuelekea Tunduma Mjini wananchi walimsimamisha na kutaka kutatuliwa kudai kuwa wanachangamoto za kiutawala.

Aidha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Joseph Kaganda yupo kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya(Halmashauri ya wilaya ya Mbeya) Mkoa wa Songwe(Tunduma TC) Mkoa wa Rukwa(Kalmbo na Nkasi) na Mkoa wa Katavi (Mlele na Nsimbo).

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.