MRADI WA ULGSP WALETA NEEMA KUBWA KWA WANANCHI GEITA

Na Raphael Kilapilo

Serikali yaboresha miundo mbinu Geita

Halmashauri ya Mji wa Geita imenufaika kwa kiasi kikubwa katika uboreshaji wa miundombinu na huduma za kijamii kupitia Mradi wa Uboreshaji Miji katika Serikali za Mitaa “Urban Local Government Strengthening Program” (ULGSP), unaosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia fedha za mkopo nafuu wa Benki ya Dunia.

Miongoni mwa manufaa makubwa yaliyopatikana na yanayotarajiwa kupitia mradi wa ULGSP katika Halmashauri ya Geita pindi utakapo kamilika ni; ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa km 18, Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa (Samina) “modern abatttoir", Uandaaji wa Mpango Kabambe wa Mji wa Geita “General Planning Scheme” (GPS), na Uboreshwaji wa mifumo ya mipango miji na ukusanyaji mapato kwa njia ya Kielektroniki.

Akizungumza na ujumbe kutoka Benki ya Dunia, OR-TAMISEMI pamoja na maafisa mbalimbali kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza mradi wa ULGSP, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinary alisema kuwa ujio wa Mradi wa ULGSP umeleta neema kubwa kwa mji huo wa Geita unaokuwa kwa kasi.

“Ujio wa mradi huu umetuwezesha mpaka sasa kukamilisha ujenzi wa barabara ya jimboni kwa kiwango cha lami ya kiwango cha juuyenye urefu wa kilomita mbili nukta mbili (2.2 km) kwa mwaka 2016/2017. Pia ujenzi wa barabara mbili za “American Chips” na Miti mirefu I & II zenye urefu wa kilomita mbili nukta sita (2.6 km) unaendelea kwa sasa”, alisema Mhandisi Apolinary.

Aliendelea kueleza kuwa ujenzi wa barabara hizo umesaisia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi kwa wananchi wanaokaa kwenye maeneo yanayopitiwa na barabara hizo; kwa kuanzisha biashara, kupanda kwa thamani ya nyumba na viwanja ambap kumesaidia kuinua kipato cha wananchi katika maeneo hayo.

“Miundombinu hii ya barabara imesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero ya usafiri na mafuriko kwa kurahisicha usafiri kwa wananchi na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali.” alisema Mhandisi Apolinary.

Aidha alieleza kuwa ULGSP imefanikisha kuanzishwa kwa Kitengo cha Ukusanyaji Taarifa kwa Njia ya Kijiografia “Geographical Information System Unit” (GIS), ambapo kumeiwezesha Halmashauri kuanzisha kanzi data “data base” ya taarifa mbalimbali zitakazo ziwezesha idara zote kuzitumia kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wananchi. “GIS imetuwezesha uthamini wa majengo na kuandaa daftari lenye orodha ya majengo yaliyothaminiwa 14,223 katika kata tano za Geita. Kwa sasa orodha hiyo inapitiwa na wananchi kwa lengo la kuhakikiwa na kabla ya kuanza kutumika. Jambo hili litaiwezesha Halmashauri kuongeza mapato yake ya ndani mara dufu na kuboresha huduma kwa wananchi,” alisema Mhandisi Apolinary.

Zaidi ya hayo Mhandisi Apolinary alieleza kuwa ULGSP imewasaidia kuandaa Mpango Kabambe wa Mji wa Geita “General Planning Scheme” (GPS), ambao kwa sasa upo katika hatua za mwisho za kuandaa rasimu yake “Draft Master Plan”. Aliendelea kueleza kuwa mpango hou utaleta mapinduzi makubwa Geita kwa kuupanga mji na kuondokana na kero ya makazi holela; umeainisha na kutenga maeneo ya makazi, biashara, viwaanda, na uwekezaji mbalimbali. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhe. Leonard Bugomola, alieleza kuwa Mradi wa ULGSP umewezesha kuwajengea uwezo watumishi na kuboresha ufanisi wa utendaji kazi kwa kuongeza ubunifu katika kupanga na kutekeleza miiradi mbalimbali na utoaji huduma bora kwa wananchi.

“ULGSP imetuwezesha kuboresha ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani na hivyo kubuni miradi mingine mingi kwa kutumia mapato ya ndani; ikiwemo ujenzi wa soko kubwa kisasa litakalogharimu takribani shilingi 2.5 bilioni na litakuwa na vizimba 144 kwa ajili ya wafanyabiashara. Pia tunajenga jengo letu la utawala, kutenga pesa za maendeleo kwa vijana na kina mama, pamoja an miradi mingine,” alisema Mhe. Bugomola. Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamiii wa Halmashauri ya Geita ndugu Majagi Mige alisemakuwa mradi wa ULGSP umesaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Geita kutokana utekelezaji wa miradi katika maeneo mengi.

Aidha alieleza kuwa ujenzi wa machinjio ya kisasa unaotarajia kugharimu takribani shilingi 2.7 bilioni kwa hatua ya kwanza, utawezesha kukuza uchumi kwa wananchi na kuongeza mapato ya ndani kwa Halmashauri ambapo takribani Ng’ombe wapatao 100 wataweza kuchinjwa kwa mara moja. Pia Halmashauri ya Geita imeanzisha Dawati la Malamiko linaloshughulikia malamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi wakati wa utekelezaji wa mradi na baadi ya mradi kukamilika ikiwemo maswala ya kimazingira na ulipwaji wa fidia.

“Ulipaji fidia kwa wananchi kwa maeneo mengi yaliyopitiwa na mradi haukuwepo isipokuwa katika mradi wa machinjio ambapo wananchi nane walilipwa fidia kwa kupewa viwanja mbadala vilivyopimwa pamaja na hati zake vipatavyo 34, ambapo kila mmoja alipewa idadi ya viwanja kulingana na eneo lake lililochukuliwa. Hivyo hakukuwa na malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi,” alisema ndugu Maige. Mradi wa ULGSP umeanzishwa na OR-TAMISEMI kwa kuboresha utoaji wa huduma za msingi katika maeneo ya Miji. Maeneo muhimu ni; kuboresha mipango Miji; kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani hasa kodi ya majengo; kuboresha usimamizi wa fedha na manunuzi; kuboresha miundominu ya Miji na utunzaji wake; na kuboresha mifumo ya uwajibikaji na usimamizi kwenye Halmashauri.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.