HALMASHAURI YA BUMBULI YATAKIWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Na. Nteghenjwa Hosseah

Mhe Jafo aagiza Bumbuli kutumia mifumo ya kielektroniki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli ya mkoani Tanga kuhakikisha inafunga na kutumia Mifumo fungamanishi ya TEHAMA iliyoko chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ifikapo Desemba 25, mwaka huu.

Mhe.Jafo alitoa agizo hilo wakati anazindua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Lililofanyika katika Chuo cha Serikali zaMitaa Hombolo nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.

Waziri Jafo amelazimika kutoa agizo hilo baada kutolewa kwa Taarifa ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhandishi Musa Iyombe kwa kuelezea hali ya Utendaji kazi wa Wizara pamoja na Halmashauri ambazo zimekwisha fungiwa mifumo hiyo kuwa kati ya Halmashauri 185 tu ndio zimefunga Mfumo huo huku Bumbuli ikishindwa kufunga kutokana na kutokuwa na umeme.

Mhe.Jafo alisema ameshangazwa na Halmashauri hiyo kutofunga mfumo huo hadi sasa kwa kisingizio cha kuwa hakuna umeme wakati zipo Halmashauri za pembezoni mwa nchi ambazo hazina umeme lakini zimeshafunga na zinatumia mfumo huo. “Haiwezekani kushindwa kufunga mfumo kwa kisingizio cha umeme wakati Halmashauri kama ya Kakonko na kwingineko wamefunga mfumo huu na wanatumia, sitaki kuamini hii Bumbuli hata kununua genereta wameshindwa” alisisitiza.

Aliitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inanunua genereta na kufunga mfumo huo kabla ya Desemba 25, mwaka huu. “Wasipofunga walete taarifa kwa Waziri mwenye dhamana kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao, haiwezekani watu wamepewa dhamana hawatekelezi majukumu yao,”alisema Mhe. Jafo

Aidha, alisema Wizara ya TAMISEMI kwa sasa ni miongoni mwa Taasisi tatu zinazofanya vizuri kwenye Utendaji kazi tofauti na awali ambapo ilikuwa ikinyooshewa vidole kwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa.

wanakuwa na mahusiano mazuri kwenye Utendaji kazi wao kwa kuwa kukosekana kwa mahusiano hakutaleta mafanikio.

“Utekelezaji wa Bajeti unataka uwepo wa mahusiano mazuri na katika utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2017/18 muangalie namna mtakavyofanya kuwepo na thamani ya fedha kwa kuwa asilimia 20.7 ya fedha za Bajeti ya Serikali zinakuja OR - TAMISEMI”, alisema Mhe.Jafo

Katibu Mkuu OR – TAMISEMI Mhandishi Musa Iyombe alisema Wizara hii ndiyo inayoongoza kwa huduma za kielektroniki. Aidha, alisema watumishi 142 wameombewa kibali cha kupandishwa vyeo. “Katika zoezi la uhakiki wa vyeti wafanyakazi wa Wizara 12 tumewaondoa kwa kughushi vyeti na pia 19 wameondolewa kwa kukosa cheti cha kidato cha nne”,alisema Iyombe.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.