WAZIRI WA NCHI OR – TAMISEMI MHE.JAFO AHIMIZA USHIRIKIANO NA WATUMISHI WA OFISI YAKE

Na. Nteghenjwa Hosseah

Mhe Jafo aongea na Watumishi wa Ofisi yake

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Watendaji wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kubadili utendaji wao wakazi ili kupata matokeo bora katika kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI mara baada ya kuapishwa amesema biashara ya kufanya kazi kwa mazoea haina nafasi na amemtaka kila mtumishi kubadilika na kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokeo tarajiwa. Waziri Jafo amesema, “ili tuweze kufikia malengo yetu kwa hatakana ufanisi wa hali ya juu naahidi kutoa ushirikiano kwa kutosha kwa Naibu Mawaziri waliochaguliwa na kuapishwa pamoja name leo hii, Viongozi wengine wote wa Wizara, menajimenti pamoja na Watumishi wote.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Joseph kakunda amesema TAMISEMI ni injini ya Nchi na isipofanya vizuri hakuna Wizara nyingine itakayofanya vizuri kwa sababu unapozungumzia TAMISEMI unagusa wananchi na mengine yote yanayofanyika katika Wizara nyingine ni kwa ajili ya wananchi hawa wa TAMISEMI hivyo ni lazima tuweke mazingira bora na rafiki ili huduma hizo ziwafikie zikiwa na ubora wa hali ya juu.

“Wizara hii ni muhimu sana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa sababu watekelezaji wa miradi mbalimbali wako katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo tukifanya kazi kwa bidii na uaminifu hakika mafanikio yatakuja kwa haraka na hilo sisi ndio tunalolihitaji katika Serikali ya Awamu ya Tano” alisema Mhe. Kakunda.

Katika mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli Wizara ya TAMISEMI itaongozwa na Naibu Mawaziri wawili ambaoni Mhe. George Joseph kakunda na Mhe. Josephat Sinkamba Kandege huku Waziri wa Wizara hii (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) akiwa ni Mhe. Selemani Said Jafo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.