NAIBU KATIBU MKUU (ELIMU) AKAGUA UKARABATI WA SHULE KONGWE

Na. Fred J.Kibano

Naibu Katibu Mkuu Elimu akagua ukarabati majengo ya shule

Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) OR TAMISEMI Tixon Nzunda amekagua zoezi la ukarabati wa miundombinu ya shule kongwe Kilakala Sekondari mkoani Morogoro linalofanywa na Kampuni ya NASUTO ASSOCIATE Co LTD ya Jijini Dsm na kujionea maendeleo ya kazi hiyo na kubaini baadhi ya changamoto ambazo ameagiza zifanyiwe kazi na Mkandarasi wa Kampuni. hiyo.

Bw.Nzunda baada ya kufungua Mradi wa TEHAMA Kitaifa alienda kujionea hali ya ukarabati wa miundombinu shuleni hapo ambapo amesema ukarabati unaofanyika ni lazima uendane na thamani ya shilingi halisi na fedha za Serikali zisipotee bure ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya tano.

Ameyataja baadhi ya marekebisho kuwa ni pamoja na kujenga kuta ndefu katika bafu na si fupi kama ilivyo, kubomoa kuta mbovu na kuzijenga, na kuziba mianya ya msingi kwa chini ambayo itaimarisha majengo.

Amemwamuru Mhandisi Mshauri wa Manispaa ya Morogoro Mama Mmbaga kuweka wazi mikataba yote kwa shule (BOQ) na kwamba Ufuatiliaji wa kina na Tathmini katika hatua zote za ujenzi zinafanyika ili kuyafanya majengo kuwa imara na ya kudumu pasipo kukarabati kila mwaka kwani ni upotevu wa fedha za Serikali.

Naye Thomas Kahugula ambaye ni Mkandarasi amesema kasoro zote atazifanyia kazi na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu na Uongozi wa shule hiyo, Manispaa na Mkoa kwa ujumla.

Zoezi la kukarabati shule kongwe limekwisha anza nchini kote na ukarabati huo utahusisha miundombinu ya shule kama vile mabwalo ya kulia chakula, majiko, mabweni, maabara, ofisi, majengo ya utawala, vyoo nabafu, stoo na miundombinu mingine ambayo ni muhimu kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.