MHE. JAFO ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MAKOLE DODOMA.

Na.Asila Twaha

Mhe Jafo atembelea Kituo cha Afya makole Dodoma
--------------------------------------------------

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo (Mb.) atembelea na kukagua hospitali ya Makole Manispaa ya Dodoma.

Mhe. Jafo alimwambia Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Makole kuwa pamoja na ziara hiyo ni kuhakikisha wametekeleza maagizo ya Serikali iliyo yatoa ya ufungaji wa mashine za kieletroniki (EFD) ili kuhakikisha mapato ya hospitali hiyo hayapotei.

Amesema hairidhishwi na ukusanyaji wa mapato yao kulingana na ukubwa na kituo hicho jinsi kinavyochukua idadi ya watu wengi na ukusanyaji wake wa mapato bado hauridhishi amesema kabla ya hapo kituo cha Makole kilikua kinakusanya kiasi cha Tsh.milioni nne lakini baada ya kufungwa kwa mashine hizo kituo hicho kwa sasa kinakusanya Tsh 9.9 kwa mwezi amesema bado kituo hicho kinatakiwa kujitahidi katika ukusanyaji wa mapato hayo kwani fedha hizo ni moja ambazao zinatasaidia katika uboreshaji wa kituo hicho.

‘’Aidha, amewataka Wakuu wa Vitengo katika hospitali hiyo kuhakikisha kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma stahiki kwa watumiaji wa kituo hicho. Mhe Jafo amesema, Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe.Dkt John Pombe Magufuli kua imetenga kiasi pesa cha kuboresha vituo vya afya 172 na moja ya kituo hicho ni pamojana cha makole ambacho kitajengwa maabara ya kisasa, chumba cha kisasa cha upasuaji, wodi ya wazazi na pharmacy ili wananchi hao waweze kupata huduma nzuri.

Mhe.Jafo pia amewapongeza wauguzi wa upande wa maabara na kuahidi kushughulikia changaamoto zinazowakabili ni pamoja na kushughulikai suala la kuongeza wauguzi lakini pia kuongeza sehemu ya maabara ambapo pia ni moja ya changamoto alielezwa katika kituo hicho.

Aidha, ameagiza vituo vya afya vilivyokwisha patiwa fedha kuhakikisha zinatumia pesa hizo kwa mujibu wa makubaliano katika uboreshaji wa vituo hivyo mpaka ifikapo 30 Desemba, 2017.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.