SERIKALI YANUIYA KULETA MAPINDUZI KATIKA ZAO LA PAMBA

Na.Nteghenjwa Hosseah

Serikali yanuiya kuleta mapinduzi katika zao la pamba

NaibuWaziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe.Selemani S.Jafo (Mb) amewataka Maafisa Ugani nchini kufanyia kazi taaluma zao na kuwajibika ipasavyo ili kuboresha Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuleta mabadiliko chanya.

Mhe.Jafo amezungumza hayo wakati wa kikao chake na Waandishi wa Habari ambapo alielelezea nia ya Serikali katika kuboresha usimamizi wa Sekta ya Kilimo hususan zao la Pamba kwa lengo la kuinua pato la mtanzania ambaye anategemea kilimo katika kujipatia chakula na kipato.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mhe. Jafo amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe.Dkt John Pombe Magufuli inadhamiria kuleta mapinduzi katika kilimo kwa kuhakikisha kuwa Maafisa Ugani wanawajibika kusimamia uzalishaji wenye tija na wanaelimisha wakulima kutumia njia bora na kisasa katika misimu yote ya kilimo.

Aliongeza kuwa wakulima wengi wanazalisha mazao yao bila kupata utaalamu kutoka kwa wataalamu waliopo hivyo,uzalishaji duni ambao haumwezeshi mwananchi kujikomboa kutoka katika wimbi la umasikini kuanzia hivi sasa Maafisa Ugani wote watapimwa kutokana na mafanikio ya wakulima walioko katika maeneo yao.

Mhe.Jafo alisisitiza zaidi kufufua kilimo cha zao la Pamba maarufu kwa jina la Dhahabu nyeupe ambacho kwa hivi karibuni umaarufu wake umepotea ndipo aliwataka Maafisa Ugani kuhakikisha wanasimamia maandalizi ya mashamba yote ya Pamba na kufahamu idadi kamili ya mimea inayohitajika kwa kila Ekari.

Aidha, amewaagiza Wakuu wote wa Idara za Kilimo kuwa na mpango kazi sambamba na mipango kazi ya Maafisa Ugani wote walio chini yake na kusimamia utekelezaji wa mipango kazi hiyo.

“kuonekana kwa mazao yaliyopandwa bila kufuata taratibukatika mashamba ya wakulima kwa Halmashauri yoyote ni dalili tosha kwamba Afisa Kilimo Mkuu wa Halmashauri ameshindwa majukumu yake ya usimamizi na ufuatiliaji na utoaji wa elimu kwa wakulima hivyo atatafutwa afisa mwingine atakayeweza kusimamia vyema eneo hilo” , Alisema Mhe.Jafo.

Pia Mhe. Jafo alizikumbusha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa asimilia 20 kwa ajili ya Kilimo, asilimia15 kwenye mifugo na asilimia 5 kwa ajili ya uvuvi kama zilivyoainishwa kwa mujibu wa mwongozo wa bajeti ya mwaka 2017/2018.

Maelekezo yaliyotolewa kuhusu usimamizi wa Kanuni bora za Kilimo yameelekezwa kuzingatiwa katika mazao mengine yanayolimwa hapanchini ili kuleta mapinduzi ya kilimo yenye tija kwa ustawi wa uchumi wa viwanda ambao ndio kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.