Serikali yaagiza Mikoa na Halmashauri zote kuwalinda Wazee dhidi ya Ukatili na Mauaji

Serikali yaagiza Mikoa na Halmashauri kuwalinda wazee dhidi ya ukatili

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa maagizo kwa Mikoa na Wilaya kusimama imara katika kuwalinda wazee dhidi ya mauaji ya kikatili yanayofanywa na watu wasio na roho za ubinadamu.

Mhe.Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua rasmi maadhimisho ya siku ya wazee yaliyozinduliwa kitaifa katika Kiwanja cha Nyerere Square katikati ya mji mkoani Dodoma.

Amesema Serikali inasikitishwa na mauaji ya wazee ambayo yamekuwa yakiendelea hususan katika mikoa ya kanda ya ziwa kitendo kinacho kinaashiria unyama uliopitiliza.

Aidha, Mhe.Jafo amekemea tabia hiyo mbaya ambayo inaharibu sifa ya nchi na utamaduni wa Mtanzania kama ilivyokuwa hapo awali.

Kutokana na hali hiyo, Mhe.Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kupitia kamati zao za Ulinzi na Usalama kuwachukulia hatua kali watu wote wanaoendesha vitendo hivyo viovu hapa nchini.

Maadhimisho hayo yamezinduliwa rasmi hii leo kitaifa ambapo wazee mbalimbali wamepata fursa ya kupimwa afya zao bure katika viwanja hivyo na kilele chake cha kitafanyika Oktoba mosi, mwaka huu.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.