Mhe. Jafo aagiza Usimamizi Mradi wa Maji na ituo cha Afya kwa Thamani Halisi ya Fedha

Na.Fred J.Kibano

Serikali yaagiza Halmashauri kusimamia mradi wa maji na kituo cha Afya

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amefanya ziara wilayani Manyoni ambapo ametembelea Mradi wa Maji Kintiku/Lusilile wenye thamani ya shilingi Bilioni 9.9 na ujenzi wa majengo mapya katika kituo cha Afya Kintinku uliotengewa milioni 500 kwa awamu ya kwanza.

Katika Mradi wa maji Mhe. Jafo ametoa maagizo ya kusimamia kwa ukamilifu mradi ili thamani ya fedha ionekane na kufuata taratibu mpya za utoaji wa fedha ambao ni kuwasilisha cheti kwa kila hatua anayofikia Mkandarasi ili aweze kulipwa lakini pia Watendaji waweze kufanya kazi pasipo mazoea ili kuleta matokeo ya haraka kwa wananchi.

“Utekelezaji wa Miradi hii umebadilika, utaratibu wa sasa ni kwamba Mkandarasi anatoa cheti analipwa fedha kwani kupitia Mfuko wa maji kuna changamoto kubwa sana, hasa katika utendaji wetu wa kazi, kasi wakati mwingine inaweza kuwa ndogo”

Aidha, amewataka Watendaji kuwatambua Wakandarasi wababaishaiji wanaolenga kupata fedha na sio ufanisi wa matokeo ya kazi lakini pia Mkurugenzi na timu yake kusimamia kazi kwa malengo tarajiwa, “Wakandarasi wengine wanapewa kazi wafanye lakini wanalenga ile fedha lakini hawana malengo ya kuleta matokeo ya kupata maji. Mkurugenzi na timu yako simamia eneo lako kwa kuhakikisha huduma tarajiwa inafikiwa”

Akitoa shukrani zake kwa Serikali Diwani Kata ya Makutupora Mhe. Jeremia Mhembano ameishukuru Serikali kwa ujio wa Mradi huo mkubwa utakaotatua kero kwa wananchi wa Kintinku na vijiji kumi na moja na kusema kwamba maji ndio kilio chao cha muda mrefu, “kilio cha wananchi ni kikubwa sana kutokana na shida ya maji, kwa hiyo ombi letu tunaomba Mradi huu uweze kufanikiwa kwa wakati na tunajua kwamba utaweza kusaidia kusukuma”

Mradi wa maji Kintinku/Lusilile unatekelezwa na Kampuni ya Network for Water and Sanitation Tanzania (NETWAS) kwa kufanya Usanifu na pia M/S Ardhi Water Wells LTD kwa uchimbaji wa visima vine na upimaji wa wingi wa maji. Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha fedha shilingi 9,967’867,000 taslimu utakapokamilika na mpaka sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni shilingi 276,265,000 kimekwisha tumika.

Changamoto zinazoukabili Mradi wa Maji ni pamoja na utolewaji wa fedha ambao huenda kukamilika kwake ikachukua takribani miaka tisa kama fedha zitaendelea kutengwa kidogo kidogo, pia upungufu wa wataalam wa maji, ukosefu wa gari la kubebea mizigo na fedha za kuendeshea ofisi.

Katika Kituo cha afya Kintinku Mhe. Jafo amejionea hali ya Wodi za kulaza wagonjwa zikiwa katika hali mbaya, mochwari ambayo haina jokofu la kuhifadhia maiti na sehemu ya kutolea dawa ambayo inahitaji malekebisho. Amewaahidi wananchi wa Kintinku kuwa Serikali tayari imekwisha wapelekea kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya.

“Tunawaletea Mradi mkubwa, Mradi ule utajenga chumba cha upasuaji, chumba cha akina mama kupumzikia wakisubiri kujifungua, maabara yenye vifaa vyote, kichomeo taka na mochwari” alisisitiza Mhe. Jafo.

Ameagiza kukamilika ujenzi tarehe 30/12/2017 na kusema kuwa jumla ya shilingi milioni 720 zitapelekwa na kwa awamu hii milioni 500 imekwisha pelekwa tayari kwa ajili ya ujenzi lakini pia matumizi ya ‘task force account yatumike’ kwa maana ya kuwatumia wazawa katika kujenga, kulinda na mengineyo ili kuokoa fedha.

“Nimetoa maelekezo kwamba ujenzi huo ukifika tarehe 30/12/2017 uwe umekamikia, nije nikute majengo yaliyokamilika na ubora unaokidhi, lakini nikusihi Mkurugenzi simamia ujenzi hapa, uwe wa ubora. Lakini zile fedha tutafanya ujenzi kwa kutumia force account kwamba tutatumia mafundi wa hapa, tutanunua vifaa hapa hapa” alisisitiza Mhe. Jafo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Manyoni amesema matumizi ya ‘task force account’ ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wanakintinku na atahakikisha anasimamia kwa karibu kazi zote za ujenzi wa majengo mpaka mwisho.

“Mimi nianze na shukrani kwa kupata hizi fedha, kukiendeleza kituo hiki cha Kintinku, niahidi kuwa ni lazima watatumika mafundi wa Kintinku katika vikundi na kwenye majengo hayo na wengine toka vijiji vingine”

Naye Khadija Yohana ambaye ni mwananchi wa Kintinku amesema kumekuwepo na uhujumu wa maendeleo ya kijiji hicho kama vile Mtendaji wa Kata ambaye amekumbwa na vyeti feki kutoweka na mabati ya kujengea shule ya sekondari na Mhe. Naibu Waziri Selemani Jafo kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Bw. Charles Fusi ambaye hakuwa na taarifa hizo kufuatilia suala hilo.

Serikali imekuwa ikifuatilia utendaji wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi wake.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.