Mhe. Jafo awataka Viongozi wa dini kuungana na Serikali kudumisha amani nchini

Na Fred J.Kibano

Mhe Jafo awataka Viongozi wa dini kuungana na Serikali kudumisha amani nchini

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amewataka Viongozi wa dini kuwaongoza waumini wao ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya tano na kudumisha amani nchini.

Akifungua semina ya siku tatu kwa Viongozi wa madhehebu mbalimbali mjini Dodoma yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biashara, Chuo Kikuu cha Dodoma Mhe. Jafo amesema anamatumaini kuwa Viongozi hao wamekutana kwa ajili ya kufanya jambo la pamoja ikiwa ni pamoja na kuwahubiria watu ambao hawana hofu ya Mungu kwa wenzao na Serikali.

“Lakini watu hawana hofu ya Mungu, mtu yupo tayari fedha zote karibu asilimia 75 ziingie mfukoni mwake na asilimia 25 tu ziingie katika Mfuko wa Serikali, Lakini pia kuna watu wanakosa maji ya kunywa, safi na salama, kuna watu wanakosa dawa, kuna watu wanakosa miundombinu ya barabara hili ni jukumu la sisi Viongozi wa dini”

Mhe. Jafo amesema mfano mzuri kuwa watu hawana hofu ya Mungu ni mauaji ya vikongwe katika mikoa ya Mwanza na Shnyanga na hivyo viongozi hao bado wana kazi kubwa ya kuhubiri upendo ili kuwa na nchi yenye amani siku zote.

Amewataka baada ya semina hiyo, mambo yote mazuri watakayoafikiana nao basi yaende sehemu nyingine pia kama mfano wa kuigwa. “Mazuri mnatakayoyafanya yanaweza kwenda sehemu mbalimbali”

Viongozi hao wa dini wanakutana mjini Dodoma ili kusali na kupata semina ya pamoja ili kuboresha mahusiano baina ya dhehebu moja na jingine. Aidha, wamemwombea Mhe. Rais dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Serikali yake kwa ujumla ili kuweza kusimama imara na kusimamia ukweli bila ya kuwa na hofu ya wanadamu bali hofu ya Mungu kwa ajili ya maslahi ya Watanzania wote.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.