Serikali yahimiza Ukusanyaji Mapato, Vita ya Dawa za Kulevya na Kuzingatia Sheria

Na.Atley Kuni

Serikali yahimiza ukusanyaji mapato Vita dawa za kulevya na utendaji wa sheria

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Mhe. Selemani Jafo, amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kuingiliana katika utendaji, kuendeleza vita dhidi ya dawa za kulevya, wakurugenzi kukusanya mapato kwa njia ya mifumo ya kieletroniki na kutatua kero za wananchi bila ya kumwonea mtu.

Akifunga mafunzo hayo yaliyohusisha Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Mhe. Jafo amesisitiza kutoingiliana majukumu katika utendaji wao. “Waheshimiwa wakuu wa Wilaya ninyi mpo kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Rais katika maeneo yenu, hivyo msifanye Interference badala yake mkafanye intrevession, Wataalam na Mkurugenzi wakisha amua kama Mkuu wa Wilaya, ni vema mkashauriana kwa hoja na kukubaliana kwa misingi ya kujenga na sio kubomoa”

Mhe. Jafo amewataka Viongozi hao kwenda kusimamia sheria, taratibu na kanuni bila ya kumuonea mtu, huku akiwasisitiza kwenda kujenga nidhamu na kutatua kero za wananchi ili kero zinazofikishwa ngazi ya Wizara zikomee huko huko kwa kuwa katika ngazi ya Wilaya na Halmashauri wapo wataalam wengi ambao wanatakiwa watumike ipasavyo. “Matatizo yatakayo washinda basi vema mkayafikisha katika Ngazi ya mkoa, sio kuwaacha wananchi wanalipa nauli zao kupeleka kero Wizarani”

Aidha Mhe. Jafo amewahimiza Viongozi hao kwenda kupambana na rushwa na dawa za kulevya katika maeneo yao, “Kapambaneni na vita dhidi ya dawa za kulevya, tunafahamu dawa zakulevya imekuwa mwiba mchungu kwa nguvu kazi ya Taifa, tukailinde nguvu kazi hii na agenda hii iwe ya kudumu katika vikao vyenu vyote vya maamuzi”, “Aidha adui Rushwa msimuache akastawi katika maeneo yenu, haiwezekani mgonjwa akakosa bomba la sindano.

Amewaagiza Wakurugenzi kukusanya mapato kwa njia ya mifumo ya kieletroniki na kuonya wale wote wanaokwepesha mifumo iliwarudi kwenye njia za kizamani, “Jiji la Dar es Salaam leo, nimpongeze sana dada yangu Zipolla (Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam), amekuwa mfano wa kuigwa kutoka Mil. 15 hadi Mil 600 ya makusanyo ya ushuru wa maegesho ambapo hapo awali wengine walishindwa, hii ni hatua yakupigiwa mfano, ajenda ya mapato iwe yetu sote”

“Lazima (value for Money) katika miradi yetu yote mkaipe kipaumbele, jana nimetoa Press na maelekezo yamekwenda tayari juu ya ukarabati wa Vituo 172 vya afya nchini kote kwa kuwa fedha hizo nimeelekeza mtumie Force Account.

Awali akitoa taarifa fupi juu ya mwenendo wa mafunzo kabla yakumkaribisha Mhe. Jafo, Naibu Waziri OR - TAMISEMI kufunga mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Afya Dkt. Zainabu Chaula alisema, “Mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, shabaha ya Wizara ni kuwapatia mafunzo ya aina hii Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa ili kuwa na uelewa wa pamoja katika utendaji wao”

Kwa upande wake akitoa salaama za Uongozi Institute, Mkuu wa kitengo cha mafunzo Kadai Singo, alisema mambo makubwa wanayotazamia mara baada ya mafunzo hayo ni pamoja na Weledi, Mbadiliko, Wilaya zibadilike lakini kupata mrejesho wa matokeo chanya baada ya mafunzo kukamilika.

Mikoa ambayo Wakuu wa Wilaya ambao wamepatiwa mafunzo hayo katika awamu hii ni Shinyanga, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Songwe, Dar es Salaam, Njombe na Iringa.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.