Serikali yatoa miezi mitatu kukamilisha zoezi la Ukarabati wa Vituo vya Afya

Na Fred J.Kibano

Serikali yaagiza kusimamia ukarabati ya vituo vya afya

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha vituo vya afya 172 nchini vinafanyiwa ukarabati na kukamilika kwa wakati kabla ya Disemba 30, 2017 ili vitoe huduma ya afya kwa jamii lengo likiwa ni kupunguza vifo vya mama na watoto.

Mhe. Jafo ametoa kauli hiyo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake juu ya Mkakati wa kukamilisha zoezi la ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wahakikishe fedha hizo zinatumika ipasavyo na kwa lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ukarabati huo unaendana na thamani halisi ya fedha iliyotolewa” pia wahamasishe wananchi kujitolea nguvu kazi katika maeneo yao ili kupunguza gharama za ujenzi na kukamilisha mradi kwa wakati.

Pia amewataka Viongozi hao kumaliza ujenzi kwa wakati, “Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanasimamia kikamilifu ujenzi huo ili ukamilike kwa kipindi cha miezi mitatu hadi ifikapo Disemba 30, 2017 kama maelekezo yalivyotolewa kwenu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya”

Mhe. Jafo amesema kupitia Wizara ya Afya Serikali imepokea fedha kiasi cha dola za kimarekani milioni 66 toka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukarabati wa vituo 103, kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI Serikali imepokea msaada wa dola za Marekani milioni 22 itakayotumika kukarabati vituo 44, na vituo vya afya 25 pia vitakarabatiwa kwa fedha za Benki ya Dunia na Mfuko wa Afya wa pamoja (Common Basket Fund) ambazo zimevuka mwaka wa fedha 2016/2017 kiasi cha shilingi bilioni 12.5

Aidha, Mhe. Jafo amesema mara baada ya ukarabati huo Serikali itaweka vifaa katika vituo hivyo na pia ramani za majengo zilizoidhinishwa na kutumwa kwao ndizo zitakazotumika. Baadhi ya shughuli nyingine za kipaumbele zitakazofanyika ni pamoja na ukarabati na ujenzi wa jengo la maabara, ukarabati na ujenzi wa Wodi ya kina mama na watoto, nyumba ya mtumishi, ukarabati na ujenzi wa jengo la upasuaji na maeneo mengine ya rasilimali fedha. Katika hatua nyingine Mhe. Jafo amewataka Makatibu Tawala wa mikoa kuwasilisha taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kila mwezi. “kila Katibu Tawala wa kila mkoa anapaswa kuwasilisha taarifa za kila mwezi za maendeleo ya ukarabati wa vituo hivyo katika mkoa wake”

Amewataka pia Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kwamba yeyote atakayekiuka hatavumiliwa hata kidogo.

“Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo vituo hivyo vinakarabatiwa wanapaswa kuhakikisha fedha zilizotolewa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo”

“Ofisi yangu haitamvumilia kiongozi au mtumishi yeyote ambaye atatumia vibaya fedha hizo au kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha ukarabati huo unakamilika kwa wakati na kwa kiwango kilichokusudiwa”

“Ofisi yangu haitamvumilia kiongozi au mtumishi yeyote ambaye atatumia vibaya fedha hizo au kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha ukarabati huo unakamilika kwa wakati na kwa kiwango kilichokusudiwa”

Huduma ya Afya kwa Watanzania ni mojawapo ya Dhamira ya Ilani ya Chama Tawala (C.C.M) ya mwaka, 2015 chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli inayolenga kupunguza vifo vya kina mama na watoto kwa ustawi wa Taifa.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.