Serikali yazindua Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma awamu ya Tano (PFMRP - V)

Na Fred J.Kibano

Serikali yazindua Programu ya Usimamizi wa fedha za Umma awamu ya tano

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Programu ya Tano ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma ambayo inaanza mwaka 2017/2018 na kukamilika 2021/2022 mjni Dodoma.

Akizindua Programu hiyo ya awamu ya tano mjini Dodoma, Mhe.Samia amezitaka wizara, taasisi na Wakala wa Serikali kwa Tanzania Bara na Zanzibar kuufanya Mpango huu kama kipaumbele chao kwenye kazi zao kubwa ili kusimamia kwa umakini fedha za Umma kwa maslahi ya Taifa.

Amesema kama Mpango wa awamu ya Tano wa Maboresho ya Usimamizi wa fedha za Umma, Serikali itaendeleza juhudi za kukusanya mapato kwa kuboresha usimamizi wa kodi na kupanua wigo wa ukusanya kodi na kuhakikisha biashara zote zilizosajiliwa zinatumia mifumo ya fedha ya kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato na sio kodi ya mapato pekee lakini pia kuchukua hatua dhidi ya wakwepa kodi.

Pia amesema katika awamu ya Tano ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP Public Finance Management Reform Programme) Serikali haitawavumilia wafanyabiashara wasiotaka kutumia mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFD Electronic Fiscal Devices) lakini itaweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara waadilifu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameziagiza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI), Ofisi za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutekeleza kazi zilizopo za mpango huo ili kufikia malengo. Mhe. Samia amewashukuru Wadau wa Maendeleo kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania kwa msaada wa kifedha na kiufundi ambao umetolewa pamoja na DfID (Uingereza), Denmark, Norway, Finland, Ireland, KfW, BTC (Ubeligiji), JICA (Japan), AfDB, USAID (Marekani), GiZ (Ujerumani), CIDA (Canada), Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.

Kwa upande wake Mhe. Selemani S. Jafo Naibu Waziri, OR - TAMISEMI wakati akitoa shukrani kwa Serikali na Wadau wa Maendeleo kwa niaba ya OR TAMISEMI amesema ameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na Serikali kuhusu matumizi ya Mfumo wa Maboresho awamu ya tano na kwamba Mikoa na Halmashauri zote zitapatiwa maelekezo yote ya mpango huu mahsusi ikiwemo kuangalia na kufuatilia thamani ya fedha.

Mfumo mpya wa fedha wa awamu ya tano (PFMEP - v) utatekelezwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara ambao unatarajiwa kusimamia vema fedha za Umma kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla na kuanzia mwaka 1988 kumekuwepo na awamu nyingine za maboresho ya sekta za fedha zipatazo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.