Halmashauri zapewa mwezi mmoja na nusu kutumia fedha za ujenzi wa ofisi zao

Na Angela Msimbira

Serikali yaziagiza Halmashauri kutumia fedha za ujenzi wa ofisi zilizotengwa

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo ameziagiza halmashauri zote nchini kutumia fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Halmashauri kinyume na hapo serikali itazihamisha fedha hizo kwenye Halmashauri nyingine.

Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisa zinatumia fedha zilizopangwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi kutumika kwa wakati ili kupunguza matatizo ya upungufu wa ofisi kwa halmashauri nyingi nchini.

’’Halmashauri Nyingi nchini zimekuwa zikipata changamoto ya kutokuwa na ofisi za kudumu suala ambalo husababisha utendaji wa kazi kuwa mgumu na kuleta adha kwa wananchi ambao wanategemea kupata huduma kutoka kwenye Halmashauri”, Mheshimiwa Jafo amesema.

Mhe.Jafo amesema kuwa Serikali ilijiwekea mkakati wa kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinakuwa na ofisi za kudumu kwa kuzitengea fedha za ujenzi wa majengo ya ofisi lakini zipo halmasauri ambazo hazijatekeleza ujenzi mpaka sasa kwa kutoa sababu zisizokuwa za msingi.

Mhe. Jafo ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi kutumika ndani ya mwezi mmoja na nusu kinyume na hapo serikali haitasita kuzihamisha fedha hizo kwenye halmashauri zilizotekeleza miradi hiyo.

Naye Meneja Kanda ya Kati kutoka SUMA JKT Meja Zabron Mahenge amemueleza Naibu Waziri kuwa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino umegharimu kiasi cha shilingi milioni 741 ambazo zitamalizia ujenzi wa ofisi kwa gorofa ya kwanza na kazi hiyo inategemea kumalizika ndani ya miezi mitatu.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Athumani Masasi amesema amepokea maagizo ya Serikali ya kuhakikisha kuwa watumishi wote wa Halmashauri ya Chamwino wanahamia ofisi mpya hadi kufikia Januari, 2017 kwani kwa sasa wamepatiwa ofisi na Mkuu waWilaya ya Chamwino lakini bado Idara nyingi zimetawanyika.

p align="justify">

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.